Uchaguzi 2020 Mtifuano mkali Jimbo la Mbeya Mjini, Ngoma inogile

Uchaguzi 2020 Mtifuano mkali Jimbo la Mbeya Mjini, Ngoma inogile

Albert Einstein

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2017
Posts
394
Reaction score
582
Habari wakuu,

Wiki iliyopita nilikuwa kwenye kampeni ya mgombea ubunge wa upinzani anayetetea kiti chake Mhe. Joseph Mbilinyi eneo la Stendi ya chunya. Nilichogundua ni kwamba kuna vijana anaotembea nao kila kona na kwa jinsi walivyo sidhani Kama anawalipa chochote (Labda ushawishi tu). Hili ni kundi linalosema tutakufa na Sugu wetu iwe isiwe na baadhi yao huenda ndio wale waliopewa mkopo wa bajaji na bodaboda kutoka kwa Tulia trust foundation na walizitumia kuenda kumpokea #ni yeye alipowasili jijini Mbeya. Na kuzitundika bendera za CHADEMA kwenye Vyombo hivyo.

NYUMA YA PAZIA
Ipo wazi kamati ya siasa ya upinzani Mbeya mjini haina maelewano kabisa, Campaign manager wa siku zote wa Mhe Sugu anaitwa Kamanda Mwambigija (Almaarufu mzee wa upako - Kiboko wa CCM mkoa wa Mbeya) wanapishana na Mhe Sugu kwenye mafao, Mwanzoni kabisa Sugu alimnunulia Mwambigija kiwanja eneo la Lyoto - Plot D (lipo mbeya mjini) na alianza kumjengea nyumba nzuri tu lakini ujenzi umesimama baada ya Sugu kuona upepo wa 2015 sio wa mwaka huu (isitoshe idadi ya wapiga kura imeongezeka mwaka huu).

Kwa wasiomfahamu Kamanda Mwambigija a.k.a mzee wa upako ndio alimnadi Sugu 2010 enzi hizo hajakomaa kisiasa na 2015 pia.
Za chini ya pazia inaelezwa mwezi February, 2020 kuna mpango kwamba mbogamboga walitaka aunge juhudi lakini sijui walishindana wapi Ila Sugu alitoka huko na kuja kusolve.

Waliopo mkoani Mbeya ni mashahidi, ushirikiano wa Mwambigija upo chini Sugu anatumia nguvu nyingi kumkebehi Dr Tulia ... Mara alikuwa anaingilia majukumu Yangu, sijui mwanamke hajaolewa yule muongo, Mara mbeya mjini sio ya kuongozwa na mwanamke... Aisee huyu sio Sugu wa 2015. Mwaka huu ngoma mzito

UPANDE WA CCM
Jana pia nimehudhuria kampeni za CCM eneo la viwanja vya Itubi kata ya Iganzo, in short alikuwa na kazi ya kuwasikilizisha wananchi clip zake za bungeni alipokuwa akiisemea Mbeya Mjini maswala ya maendeleo (wakati Sugu alipotoka bungeni kwa amri ya Mr Dj). Dokta anadai yeye ana connection ana simu ya mzee dingi na pia mzee dingi anayo yake.. pia ameeleze mikakati yake na Tulia trust alivyofanikisha miradi kadhaa ya maendeleo.

(Hapa sijajua fedha za Tulia trust zinatoka wapi) Ila mikutano ya Tulia ina watu wengi na Wana positive responses.

Hitimisho;
Kimsingi hili jimbo bado gumu kwa CCM. Kuna watu hata uwaeleze nini bado kura ni ya Upinzani namshauri Sugu ayaweke sawa na kamati ya siasa ili October iishe vizuri

"Maendeleo hayana vyama"
 
Kwa sisi ambao tupo Mbeya wala hatuoni huo mtifuano

Mikutano ya Tulia watu wanabebwa kutoka Chunya Busokelo na wilaya nyingine...

Juzi hapa kaja Samia watu tumeruhusiwa kutoka kazini saa mbili asubuhi ili tukajaze mkutano!

Tulia anajuta kwanini alichagua Mbeya mjini baadala ya kwa SAULI
 
Kwasisi ambao tupo mbeya wala hatuoni huo mtifuano

Mikutano ya Tulia watu wanabebwa kutoka Chunya Busokelo na wilaya nyingine...
.
Upo sahihi mkuu huyu tapeli anaeneza taarifa za uongo, mimi nipo Mbeya wiki ya 2 sasa sijaona hicho kitu
 
Mwaka Atapata Tena Kura 100000 Na Zaidi
 
Wacha utani mjomba, huyo Mwambigija kama anakubalika sana kwanini yeye asigombee huo Ubunge hapo Mbeya Mjini?
 
Kumchagua TULIA kwa Mbeya ni kujidhalilisha wenyewe wana Mbeya. Huyu kigagula kwanza hakubaliki hata Rungwe ndiyo maana akakimbilia Mbeya.

Halafu kwa nini tuchague mbunge anayedai AMETUMWA na Magufuli?
 
Back
Top Bottom