Mtihani hatari katika maisha ya binadamu

Mtihani hatari katika maisha ya binadamu

Kaunara

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2013
Posts
249
Reaction score
452
Moja ya mtihani hatari katika maisha ya binadamu ni kufaulu KUOA / KUOLEWA na mtu sahihi. Ukifeli hapa hutaichukia hata elimu yako hata kama ni PHD. Unaweza chukia hata kwanini hupo duniani.

Wengi wamejaribu kufanya masahihisho ya mtihani huu ila wanahangukia pua. Bado amani ya moyo inakuwa hamna.

Kama kuna jambo linahitaji utulivu, hekima, akili na Mungu katika maisha ya duniani ni kuchagua mtu sahihi katika maisha yako.

Binadamu kapewa mda mrefu sana wa kuchagua mtu wa kuoa au kuolewa nae. Kuanzia Elimu ya primary, secondary hadi chuo.

Wengi hujua wamekosea kuoa au kuolewa pale ambapo wanakuwa tayari wana mtoto au watoto na hapo ndo rangi kamili za kila mmoja wao huonekana wazi bila kificho. Hapo ndo unajua Singeli hii inachezeka au haichezeki.

Kwa wewe unaesoma huu uzi na bado hujaingia kwenye huu mkasa aisee anza kumpima mtu wako sio kwa mazuri tu hata mabaya angalia reactions zake. Hakikisha unaichimba vizuri background ya mtu pamoja na familia yake usikurupike. Achana na rangi, shepu au sura. Ukichemka aisee hata hiyo rangi utatamani kuiona. Mshirikishe sana Mungu wako katika hili hamna ujanja.

Kiasharia kibaya kwangu mimi katika mtihani huu. Ni ULEVI WA AINA YEYOTE ILE. Angalia sana mwenzako ana ulevi gani, kila mmoja chini ya hili jua ana ulevi wake. Na siku zote ulevi kwa mtu uongezeka na sio kupungua. Mfano mtu alikuwa anapiga kreti la bia usidhani akiwa baba au mama hatapunguza. Graph yake ni increasing at increasing rate hapo lazima ukae sawa. Kuwa makini sana pale ulevi wako unapotaka kumfundisha mwenza wako jua kabisa kuna siku utakugharimu ukimfundisha.

Pia siri za familia yako kaa nazo kimya usianze kuropoka siri za familia uliyotoka kwa mpenzi wako mambo waliyokosea wazazi wako kufa nayo. Mpenzi wako bahati mbaya akiona udhaifu katika familia yenu aone yeye kama yeye sio wewe kumwambia itakua ni fimbo badae kwako.

Waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu. Fanya masahihisho pale unapoona mawingu na sio mvua. Ni gharama sana kumtambulisha mzazi watu wawili au watatu katika maisha yako. Ni wazazi wachache sana wanaweza kukwambia ukweli ila wengi pale unapojaribu kufanya masahihisho wanajua ushafeli.

Mara nyingi mtu wa kwanza kumleta kumtambulisha nyumbani uwa anabeba na baraka fulani za wengine ambao watakuja nyuma yake kama itatokea ingawa sio kwa wote.

Kwa wewe ambaye unaona mtihani huu ushafeli na unataka kurudisha mpira kwa kipa ushauri wangu marekebisho pia yatakugharimu sana. Maana jua kabisa uwe mwanaume au mwanamke utavua au utavuliwa sana pichu hadi akili ikae sawa tulia

Moja ya nyenzo ya kushinda mtihani huu kama una hisi umekosea basi hujachelewa kaa kimya kuanzia leo. Pale unapoana unahisi unataka kujibu, kutukuna au kupiga basi kausha kaa kimya kuna vitu utarekekisha au puuzia mambo au maneno mabaya kwako, kama kuna ushindani basi kaa kimya pale unapotakiwa kujibu ni bora ukasema sijui kuanzia sasa.

Ukitaka kujiona we ni mjuaji sana kuliko mwenzako hutajua chochote ni bora ukajiona hujui sababu utajua mengi.Pia Neno samahani na kujishusha pale unapokosea ndo ushindi katika mtihani huu, badilika kuanzia sasa utakuja kunishukuru.

Unavyoamua kuishi n mke au mume jua kabisa umesign mikataba mingi sana ambayo mambo yasipoenda sawa inaweza kukugharimu kama kuua, kuishia jela, kuwa single parent siku moja, kuuwawa pia, kusalitiwa kudhalilishwa, kuishi kama watani wa jadi ndani na mengine mengi lazima ujiandae sana kisaikolojia. Haya yote yanaendana na jinsi utakavyochukulia mambo katika mtihani huu.

Mwisho na watakia maisha mema na pia nawapongeza wale wote ambao wanaishi kwa furaha na kuwa mfano au kioo katika jamii yetu Mungu awabariki sana.
 
Mwakani nafungua chuo cha kutoa short course zinazohusu hilo somo. Mwanafunzi atakayefel atarudishiwa pesa yake.
 
Back
Top Bottom