Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa

ocd

Member
Joined
May 3, 2013
Posts
6
Reaction score
3
Jana mheshimiwa Rais wa Tanzania alizindua Sera mpya ya Elimu ambapo kati ya mengi yaliyomo ndani ya sera hiyo ni kufutwa kwa mtihani wa Darasa la Saba na Elimu ya Msingi kuongezwa hadi Kidato cha Nne.

=========

Source: The Citizen
 
Duh!

Kwa hiyo form 5 na 6 inakuwaje? Kwenye kiswahili, binafsi siungi mkono! Hatuna vitendea kazi BADO vya kufundishia kiswahili mpaka chuo. China, Korea, Uk, USA walifanikiwa kwenye lugha zao mama kama lugha za kufundishia sababu walikuwa na rasilimali ya kutosha, na kikubwa uwezo wa kifedha.

Ila ngoja tuone, tuwe positive!
 
Sidhani kama tutafanikiwa katika hili.
 
Upuuzi wa hali ya juu huu.

Rwanda wameongeza kiingereza sisi tunapunguza lugha. Katika hao rais, waziri wa elimu, katibu mkuu watoto wao wanasoma njee halafu wanawadanganya watanzania
 
BONGOLALA

We produce what we don't consume and we consume what we don't produce!
 
Last edited by a moderator:
Majanga,

Najiuliza tu ma-housegirl... mimba nk miaka saba tu shughuli sasa unaweka mpaka form four.., saidia fundi watapatikana wapi? Mi mawazo yangu ni kuwa na wasomi haswa na kuwa vocational skilled labour force haswa.

Hivi ni shule gani za msingi cum secondari zitakazoweza kuwafundisha elimu ya ufundi haswaaa. Vifaa watavipata wapi?Bunsen burner tu wameshindwa kununua je wataweza kununua lathe machine?

Nilifikiri elimu ya msingi iwe mpaka darasa la tano, then unakuwa na wale wanaoenda michepuo ya vocational na wale wanaoendelea na pure shule hivyo hivyo mpaka secondary, na iwe compulsory.

Tatizo letu sasa tuna wasomi wavaa tai wasiojua kufunga tai. Graduates weeengiii lakini weupeeee , matokeo yake wachina wanakuja na nyundo za kunyoosha magari na wanapiga hela ya hatariii.

Dah, yani mi hata sielewi dunia watakayoishi watoto wetu.
 
Upuuzi wa hali ya juu huu.

Rwanda wameongeza kiingereza sisi tunapunguza lugha. Katika hao rais, waziri wa elimu, katibu mkuu watoto wao wanasoma njee halafu wanawadanganya watanzania

Nchi hii mungu aiumbe na viumbe wapya, otherwise?
 
Sera ingine ya hovyo hovyo kabisa!!
Kama vile KILIMO KWANZA au BRN hata hii itashindwa tu maana haina maandalizi yyt ile
 
Sasa udhaifu mkubwa uliopo shule za msingi utahamia sekondari. Tutabaki na taifa tepetepe kitaaluma. Sera hii ya elimu ya Prof. Dr. Kikwete siiafiki kabisa. Eti kiswahili ni medium of instruction from primary school to university! Vitabu vya kiada kwa kiswahili vimetunga au kutafsiriwa lining? Au kila mwalimu atafsiri anavyojua?
 
barafuyamoto

Tanzania ni kichwa cha wendawazimu na kila siku wanazidi kuongezeka kipofu akimwongoza kipofu wote......
 
Last edited by a moderator:
wamelileta hili wakati muafaka kabisa, hii ni sababu tosha kabisa ya kuwaondoa hawa wehu.
 
Hiyo Policy yenyewe utakuta imeeandikwa kwa kiingereza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…