Wakubwa ni kwamba pepa zinavuja kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu, na hii kitu haijaanza leo. Kilichobadilika ni teknolojia ya habari tu, kwa hiyo hata wasio kwenye mtihani wanapata habari. Zamani hizi habari ziliishia huko mashuleni, na wale ambao hawajafanya mtihani walitunza siri ili hiyo "channel" ya pepa iendelee kudumu zamu yao ya kufanya mtihani ikifika nao waitumie. Mitihani ya kuvuja ilikuwa na majina mengi kama "nondo", "kirungu", kule chuo kikuu mlimani waliita "desa", Muhimbili waliita "mwezi" nk.
Wavujishaji wakuu wa mitihani wako katika makundi kadhaa:
1. Wafanyakazi wasio waaminifu wanaotaka kujipatia fedha kwa kuuza mitihani. Hawa wako katika sections mbalimbali katika process ile ya kuandaa mitihani kuanzia uchapaji, kurudufu, kufungasha, kusafirisha nk. Na hawa ni ngazi zote, shule ya msingi hadi university. Uzuri ni kwamba hawa ni rahisi kuwadhibiti kwa kuziba mianya yote na kuweka kanuni za usalama zinazozingatiwa na zinazoji-monitor zenyewe.
2. Kundi la pili ni la wamiliki wa mashule na wakuu wa mashule wanaotaka kujenga sifa kuwa shule zao ni bora. Hawa hununua mitihani kwa gharama yoyote na kuifundisha mashuleni, na wala huwa hawaoni aibu kuwaambia wazazi waongeze michango ya "special tuition" kwa ajili ya watoto wenye mitihani (form 2, 4, 6). Kinachowawezesha hawa kufanikisha hii ni kupenyeza vigogo wa baraza la mitihani kwenye payroll za shule zao, kwa hiyo hizi paper zinatoka kwa wakuu wa Baraza la Mitihani, wale wenye dhamana ya mwisho kabisa ya kuaminiwa (actually wale wanaodhibiti wizi wa mitihani ndio wanaopelekea hawa jamaa hizo pepa). Mitihani ya namna hii inapovuja si rahisi kuonekana mizimamizima maana wahusika huwa wanakabidhi maswali kwa waalimu wa masomo, ambao wanayafundisha darasani kama "revision" za kawaida, kwa hiyo si rahisi kuwastukia. Tatizo linatokea wanapomkabidhi mwalimu paper nzima na yeye ana tamaa ya pesa, anauuza kwa dalali (au madalali) ambao wanaanza kuutembeza kama njugu, hapo ndio "soo" linabumburuka!
3. Kundi la tatu ni wazazi wenye influence huko baraza la mitihani ambao wanaiba mitihani hiyo kwa ajili ya watoto wao. Hawa pia ni vigogo, na huipata kutoka kwa vigogo wa baraza. Anapofikisha mtihani nyumbani anamkabidhi mwanae anamwambia "ushindwe mwenyewe sasa!" Ikitokea mtoto hajiamini, anatafuta rafiki (au marafiki) anaoamini ni "kipanga" katika kila somo ili wamfundishe (siri imeanza kutoka hapo). Wakimaliza kufundishana, wanakumbuka "unajua tunaweza kutengeneza hela hapa?" Wanaanza biashara kuuzia wenzao.
Udhibiti wa mitihani unatakiwa uanze kwanza na vigogo wa baraza la mitihani, maana hawa wengine wa chini wanaumiza vichwa kulinda mitihani ambayo ilishavuja kabla hawajakabidhiwa!
(BTW hii ndio ilikuwa proposal yangu ya awali kwa ajili ya tasnifu yangu ya masomo ya uzamivu, lakini kutokana na "siasa" zilizomo ndani yake niliiacha maana uwezekano wa kuifanikisha ulikuwa mdogo sana. Changamoto kwa anayeipenda aichukue, awe jasiri!)