Mtihani wa Taifa kidato cha pili bila kurudia una maana?

Mtihani wa Taifa kidato cha pili bila kurudia una maana?

EDOARDO

Senior Member
Joined
Oct 4, 2010
Posts
114
Reaction score
13
Wadau. Mi naona sasa ni wakati muafaka wa kujadili kwa kina kuhusu mtihani wa kidato cha pili kuendelea kuitwa wa Taifa. Hivi una mantiki kweli! We jiulize kama wanaenda wote kidato cha tatu pamoja na waliofeli kuna haja tena ya mtihani huu au ni matumizi mabaya tu ya fedha na rasilimali watu? Chagieni wadau!
 
Huu mtihani kitaifa ungefutwa ila kila shule inatakiwa kuangalia jinsigani ya kuwapima wanafunzi wake.
 
kwa mtazamo wangu-serikali imefanya jambo la kijinga sana kufuta mtihani wa kidato cha pili,maana ulikuwa unajaribu kupunguza zero form four,ila kwa sasa zero lazima ziongezeke sana maana ni fulu tambarare kwa wale wote ambao walitakiwa kubakia form two
 
Hakika mtihani wa kidato cha pilli ni muhimu sana na umuhimu wake na maana yake ni wale wanaopata chini ya alama kurudia mwaka,wanafunzi wa kidato cha pilli inabidi wasome kwa kuogopa ki2 flan ili waweze kuendana na elimu pamoja na balekhe katika hali ya usalama na mtihani wenyekurudia ndio ki2 cha kuwapa fear na hivyo ku2mia muda wao mwingi kwenye masomo kuliko kwenye matatizo xa balekhe na pia kuwajengea tabia ya kujisomea na kuwafanya kuwa bora.KUFUTA SYSTEM YA KURUDIA NI KUCHOCHEA BORA ELIMU NA SI ELIMU BORA NA ZAIDI KUSABABISHA MATATIZO KWA WAZAZI NA WALEZI WA WANAFUNZI..
 
Sasa nini kifanyike? Maana ni kweli wanafunzi wa kidato cha pili siku hizi wanaonekana wakijiachia tu na kutokuwa na hofu yeyote. Hivi kweli zero fm 4 zitapungua?
 
mimi na-support kutokurudia baada ya kufeli mtihani wa kidato cha pili. hiyo ni indicator nzuri both kwa mwanafunzi na kwa mzazi wake juu ya nini wategemee kwenye matokeo ya f4. kwa kipindi cha miaka 3 inayobakia wakichukua hatua wanaweza kubadili upepo wa iendako merikebu yao! mtihani wa f2 uchukuliwe kama mock exam, ambayo iko serious na imitating ule wa f4! kwa kurudia kama ni kilaza haitaleta mabadiliko. actually ni kuwasonga tu wa nyuma yako. jamani,tuwafundishe watoto wetu kuwa unavuna unachopanda!kwa hiyo wakipanda bangi wasitegemee kuvuna mchele!
 
Jamani ndg zangu watanzania 2cpotoshe jamii kwa kuongelea 7bu ziczo na tija, 2jiulize maswali yafuatayo
1. Je cc kipindi 2po shule 2liufanya mtihani huo unaoitwa kidato cha 2 kitaifa, ikiwa haifanani na watahiniwa hao kwa nchi nzima?(mtihani wa kikanda kwa kdt cha 2)
2. Je nini kipimo cha waloyalosoma kwa wahusika ikiwa hakuna mtihani wenye kuleta tija kwa masomo yao?
3. Kipindi cha haki za binadamu kilichopamba moto kuwatetea wanafunzi kuhusu kutochapwa, kutofanya kazi zozote shule ikiwa hata kufagia darasa lao wenyewe, kumwagilia na kudhubutu kuwatetea waje na cmu shuleni na kuingia nazo darasani kwa kisingizio kutokua na sheria ya kudhibiti matumizi ya cm ktk mazingira niloyataja? Tunakwenda wapi? Halafu 2waondolee mtihani wa kuleta heshima, wa kuwafanya wakumbuke kuhusu kilichofundishwa kinatakiwa kufanyiwe kazi?

Jamani ndg zng ni vyema kuyafanyia kazi 2cfikie kipindi 2kasema hata mtihani wa kidato cha nne, 6 na chuo iondolewe ikiwa mtihani wa darasa la 4 unakomaliza. 2fikiri kwa mapana, chonde chonde 2cielekeze nchi huko, ni vyema 2kaangalia madhara yake c urahic tu.
 
Sasa nini kifanyike? Maana ni kweli wanafunzi wa kidato cha pili siku hizi wanaonekana wakijiachia tu na kutokuwa na hofu yeyote. Hivi kweli zero fm 4 zitapungua?
<br />
<br />

Kwa nini wewe usijibu unavhofikiri na kuacha kuuliza maswali kama vile unahitaji msaada kwenda kujibu mahala

Unataka fikra zetu ikusaidie sasa nawe JIBU tusome yako...the teh
 
Kwa shule zilizo makini tangu zamani zina wastani wao kila mwaka wa kuvuka kidato na wala hawakuwa wanaufata wastani wa serekali wa kidato cha pili kwa hiyo unakuta mtu kafaulu wastani wa taifa lakini amefeli ule wa shule basi lazima arudie au ahame sasa hii ndio safi na nadhani ili shule iwe bora kwa matokeo ya kidato cha nne inabidi ifanye hivi la sivyo itatengeneza zero za ajabu maana mitoto ya sasa hivi na hasa uku uswahilini ni bure kabisa kazi usista du na usharobaro plus mapenzi na mbaya zaidi vingi vinasoma shule za kata na hata kama sio za kata basi utakuta ni zile za viwango duni sa sa sijui watavuna nini na serekali yao ya kipumbavu!
 
1.>>Kwanza ifahamike kuwa hakuna mtihani wa kidato cha pili 'kitaifa' -- kila kanda ya elimu hapa nchini ina mtihani wake tofauti. Wame-standardize tarehe tu mitihani hii inapopaswa kufanywa.
2.>>Kwa sasa mtihani huu ni kwa ajili ya kujaza CA -- continuous assessment kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne. Ni kama uthibitisho hivi kuwa mtahiniwa huyu amehudhuria shule, alama atakazozipata ni muhimu katika kumdhibitisha kama mtahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne.
3.>>Kipi ni bora kati ya kuziba jino lililotoboka au kuling'oa? Kuwafanya wanafunzi wakariri darasa sidhani kama inawasaidia ku-improve kama hautafanaya jitihada zozote za kukabiliana na visababishi vya mwanzo vilivyopelekea kufeli kwake. Sioni mantiki ya kukariri darasa kwa anayefeli kama hatutatengeneza mfumo madhubuti wa kuwasaidia.
4.>>Usimamizi mbovu wa kikanda pia unasababisha kiwango cha ubora wa mtihani huu kuwa chini; utunzi mbaya wa maswali, usahihishaji mbovu na wakulipua tu, n.k. vinajitokeza kwa wingi tu. System inahitaji overhaul, commitment ya curriculum planners, REOs, DEOs (S), na walimu hasa wale wanosimamia zonal exam sysndicates katika kuhakikisha kunakuwa na mitihani madhubuti yenye ubora na malengo dhabiti ya kumpima mwanafunzi wa kidato cha pili.
 
Darasa la 4 la mkoloni ni sawa na form 4 ya leo ya mwanafunzi wa tanzania!elimu yetu haina muelekeo we looking on quantity not quality!
 
Ok. Mkuu nashukuru kwanza kwa kutaka kujua mawazo yangu. Mi kwa mtazamo wangu naona kuwa mtihani wa kidato cha pili ni muhimu sana, na wanaofeli warudie darasa ili kupunguza zero form 4. Na si kweli kwamba naenda kujibu mahali, isipokuwa ni jambo ambalo limenigusa kama mdau wa Elimu.
 
Back
Top Bottom