Mtihani wa uelewa wa elimu ya fedha

pipi34

Member
Joined
Apr 16, 2018
Posts
5
Reaction score
6
*MTIHANI WA UELEWA WA ELIMU YA FEDHA*

kabla sijaanza kufundisha juu ya elimu ya fedha naomba kutoa mtihani huu wa kifedha, lengo la mtihani huu Ni kujitambua wewe mwenyewe juu ya uelewa wako wa mambo ya kifedha au nafasi yako katika elimu ya fedha katika mtihani huu utakuwa ukijibu *NDIO* , *HAPANA* au *SIJUI* kwenye kila sentesi ambayo inaandikwa hapa kwa urahisi zaidi unaweza kuchukuwa daftari ukaandika huu mtihani na ukaanza kuwa unajaza na mwisho wa siku mkimaliza wote mtaniambia jioni nije nielekeze ili uweze kujua kiwango chako cha elimu ya fedha kikoje. Kila Mtu afanye kwa wakati Wake na jioni kwa watakaoweza kila Mtu anaweza kutushirikisha alichokifanya

*MASWALI YA MTIHANI*

1.Je unafahamu hali yako ya uchumi kwasasa au kiwango cha utajiri wako kwa sasa? *NDIO* , *HAPANA* , *SIJUI*

2.Je! Umeridhika na hali ya uchumi wako wasasa? *NDIO*, *HAPANA*, *SIJUI*

3.Je unafahamu njia za kukufanya kuongeza kipato chako?

4.Je umeshajiwekea akiba ya kutosha ambayo hata ukifukuzwa kazi leo au ukiugua miezi sita unaweza kuishi bila tabu?

5.Je unajiwekea akiba za kutosha kwenye kikundi chako mara kwa Mara?

6.Je unamalengo YA kifedha (yani umeshapanga unataka kuingiza kiasi gani kila Mwezi)

7.Je unaaccount bank yakwako binafsi?

8.Je unatabia ya kuchukuwa bank statement yako kila mwezi kuhakikisha unakagua kipato chako ulichoweka kwa mwezi au unaangalia kitabu chako cha vicoba

9.Je unatabia ya kuandika mapato na matumizi yako ya kila siku?

10.Je unafahamu kiasi gani unatumia kila mwezi?

11.Je unatumia kiwango kidogo zaidi ya unachoingiza?

12.Je unabajeti ya matumizi ya familia yako kwa mwezi? Na je unaifata?

13.Je unauwekezaji wowote ambao umeshaufanya hadi sasa?

14.Je unamshauri wa kifedha?

15.Je unajua watoto wako watasoma shule gani hadi chuo kikuu?

16.Je unaridhishwa na mchango wako kwenye maisha ya watu wengine?

17.Je umejipanga kwa maisha yako ya kesho?

18.Je umeshafikiria ikifika wakati wa kustaafu utakuwa na utajiri wa kiasi gani?

19.Je unanyumba?

20.Je unafikiri kiasi unachowekeza na kipato chako nisawa

*HAYA KILA MTU ANAYONAFASI YA KUFANYA HUU MTIHANI WEWE MWENYEWE BINAFSI MKIMALIZA NIAMBIENI, KILA MTU ASEME TU NIMEMALIZA, HALAFU BAADAE NITAKUJA KUELEZEA KUWA UKIPATA HAPANA NGAPI UTAKUWA NA LEVEL GANI NA UKIPATA NDIO NGAPI UTAKUWA WAPI*
 
hapo mtu ndio anajazaje boss? tumia yahoo au google questionare creator
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…