Mtikila atupwa rumande! Demokrasia itapatikana?


well said Mkuu FMES!!! kesi ikiwa mahakamni hatuna sababu ya ku-conclude mara upinzani wanafungwa demokrasia iko wapi.... na sidhani ni busara kuanza kulaumu!!!

Mtikila angetimiza masharti ya dhamani basi angetoka asubirie kesi yake na maamuzi ya mahakama.

so far he is still innocent until proved guilt!!
 
Wapigania haki siku zote wawe tayari kupitia njia hii kwa kila sababu, iwe ina sound vizuri kwenye masikio ya maadui au la. Kwa kila sababu wote mnaopigania haki ndiko muwe tayari kupitia. Na njia hii haitawahi kuwa ya mtikila pekee maana wengi wamepitia njia hii na sababu zilikuwepo na sababu hazitakosa. Lakini ole wake adui atakapojiliwa....... kiburi kitakoma.
Siku moja mtakumbuka maneno haya.
 
Siasa ndiyo hizo!! aliyeshikilia dola si mwenzako. Mtikila ajichunge, na aepuke kutusi walio katika enzi!!
 
Ukichunguza sana sheria imefuata mkondo wake ila huyu Mchungaji alikiuka vifungu vya sheria.Sijui alifanya hivyo kwa kudhamiria au ndiyo katika kutaka kuandika historia?
 

Demokrasia ni Mtikila na Kulikoni tu?
 
May be yule nyoka aliyemgonga siku ile kule Zimbabwe alilegeza some brain attachment za Mtikila, vituko vyake vimeanza!
 
Wana JF, kheri ya mwaka mpya. Nilijiunga na jukwaa hili muhimu, majuma mchache yaliyopita, lakini bado nilikuwa sijawasiliana nanyi rasmi kwa vile nilikuwa kwanza nikipitia michango yenu, makala, na habari nyingi za kusisimua. Shukrani nyingi kwa michango yenu muhimu na ya kuelimishana.

Ningelipenda kusema chochote kuhusu mashtaka yanayomkabili Mchungaji Mtikila. Katika demokrasia ya kweli, watu hawashtakiwi kwa kuwaita viongozi walio madarakani 'gaidi'.

Siku za nyuma nilishuhudia Rais George Bush Jr, akiitwa 'gaidi' kwa kujihusisha kwake katika vita vya Iraq; na, ingawaje baadhi ya watu waliomwita hivi ni Wamarekani, hawakufunguliwa mashtaka yoyote.

Dhahiri, lugha aliyoitumia Mchungaji Mtikila haikuwa na diplomasia. Lakini huwezi kutegemea watu katika jamii ya kisiasa kuwa na mtizamo wa namna moja; au hata malezi yanayolandana, kwa vile jamii nzima haitoki familia moja.

Kutumia au kutotumia diplomasia katika mawasiliano baina yetu katika jamii, ni jambo la hiyari tu, ambalo haliwezi kulazimishwa kwa nguvu za kisheria. Nina hakika kifungu cha sheria kilichotumika kumfungulia mashtaka Mchungaji Mtikila, hakiendi sambamba na wakati tuliomo hivi sasa, wa demokrasia.

Isitoshe, Rais akiitwa 'gaidi', tamko kama hili, hakika, alimfanyi Rais kuwa 'gaidi' hata kidogo.

Nje ya hilo, tamko kama hilo halimjengei chuki Rais kwa wananchi, kama chuki haipo. Badala yake, inawashangaza walio wengi kumshtaki Mchungaji Mtikila kwa kosa la 'kumtukana' Rais wakati mafisadi-papa wanaendelea kulindwa na uongozi wa kisiasa uliopo hivi sasa madarakani.

Hata mtoto mdogo, anaweza kubaini kuwa ili la mwisho linaweza kumjengea chuki Rais na wananchi wake kuliko 'matusi' ya Mchungaji Mtikila.

Kuwa Rais, kunahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana kutokana na madaraka mengi katiba inayomlimbikizia Rais. Ni uvumilivu wa namna hiyo methali ya 'Mkubwa ni jaa' inayolenga kuimarisha.

Aidha, serikali inamshitaki Mchungaji Mtikila kama fundisho kwetu wote kwamba, viongozi wetu wateule wanastahili wakusifiwa na kutukuzwa daima, jambo ambalo hata hivyo haliendi sambamba na dhana ya demokrasia tunayokusudia kujenga.

Kama madhumuni ya kumshitaki Mchungaji Mtikila yamejificha nyuma ya pazia hili, basi kama alivyonena MCHUKIA UFISADI 'Wapigania haki siku zote wawe tayari kupitia njia hii...' (ya kutupwa gerezani kutokana na kesi ambazo chanzo chake ni siasa). Hili si jambo zuri katika karne ya ishirini na moja au kwa mshikamano wa Taifa letu.
 
tuache sheria ichukue mkondo wake akuna aliye juu ya sheria but ifanye ivyo kwa mafisadi na walosaini mikataba mibovu
 
Aise Mr. Frsoty mbona avatar yako na ya ngoma nzito zinafanana?
 
ametumwa kuwahubiria wafungwa habari njema, ili baada ya uchaguzi, raisi mteule akiwatoa kwa msamaha, basi wawe wanamjua yesu na kuacha maovu,
maana wengi wa wafungwa dar es salaamu ni wale wanaodai Yesu si Mungu huku wakiwaibia watu simu zao hasa maeneo ya mwananyamala, keko, tandika, buguruni,tandale , hawa ni kina mudi guy, mudi boy, side boy, j4, dulayo, dul one, dula, sheby, sheby one sheby guy
 
tuache sheria ichukue mkondo wake akuna aliye juu ya sheria but ifanye ivyo kwa mafisadi na walosaini mikataba mibovu


Mafisadi wako juu ya sheria. Hata mkibisha ndivyo ilivyo.
Wa Richmond walishawekwa hata rumande? zaidi ya Gea tu who was just a front. wengine je? na kesi hata ya Gea imekaaje? achana na propaganda za rangi ya njano na kijani.
 
mtikila ni mkorofi sana

hapana siyo mkorofi ni mtafutaji tu kama watafutaji wengine, ndiyo maana ni mchungaji, mwenyekiti wa chama cha dp. Mpigania haki za wanyonge, mwanasiasa n.k.

Ila sijui kanisa lake linaitwaje na liko wapi.
Uko kote anatafuta maslahi, ndiyo maana ra alishawahi kumnunua. Mtikila alikataa kununuliwa na ra, siku ra alipokuja na vocha yenye sahihi yake mtikila akalala mbele.
Kwa mtizamo wangu namuona kama mtafutaji zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…