Mtikila kupandishwa kizimbani...

MalaikaMweupe

Member
Joined
Feb 24, 2009
Posts
72
Reaction score
18
Nimesikia juu juu kuwa Mchungaji Mtikila atafikishwa mahakamani leo muda wowote, kuna mtu ana habari hizi na anajua hasa amekosa nini this time?
 
Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (45) leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi wa mkoa wa Mwanza kujibu mashitaka sita.

Mtikila anadaiwa kutoa taarifa za kugushi zilizolenga kupatiwa kibali cha kuitisha mkutano katika eneo la Magomeni Kirumba.

Mtikila na mchungaji mwenzake, Eliud Rwehumbiza(41) wa jijini Mwanza wanadaiwa kutoa maelezo ya uongo kwa nyakati tofauti kwa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow.

Wakili wa Serikali, Judith Nyaki amedai kwamba Agosti 6 mwaka huu saa 7.45 mchana, Rwehumbiza aliwasilisha barua ya uongo kwa Rwambow, akionesha kwamba yeye ni Mwenyekiti wa Democratic Party ili aweze kupatiwa kibali cha kuitisha mkutano.

Imedaiwa mahakamani kwamba, Agosti sita mwaka huu,saa 9.15 Mtikila akiwa katika ofisi za Kamanda Rwambow, alitoa barua yenye maelezo ya uongo ikimtambulisha Mchungaji Rwehumbiza kuwa ni Mwenyekiti wa DP mkoa wa Mwanza.

Nyaki alidai mahakamani kuwa,barua hiyo ilimshawishi Kamanda atoe kibali cha mkutano jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa kifungu Namba 342 cha Kanuni ya Adhabu.

Shitaka la tatu linamhusu Rwehumbiza, kwamba Agosti 6 mwaka akiwa katika mazingira yasiyofahamika, wilayani Nyamagana, Mwanza, alijitengenezea nyaraka za kughushi zilizomtambulisha kama Mwenyekiti wa

DP mkoa wa Mwanza kwa lengo la kupata kibali cha uendeshaji wa mkutano.

Katika shitaka la nne, Mtikila anadaiwa anagaiwa kugushi barua ya kumtambulisha Mchungaji Rwehumbiza kuwa ni Mwenyekiti wa DP mkoa huku akifahamu si kweli.

Mahakama imeelezwa kuwa Mtikila alitenda kosa hilo akiwa katika Wilaya ya Nyamagana, sehemu isiyojulikana.

Kwa mujibu wa Nyaki, kosa hilo lililofanywa Agosti 6 mwaka huu ni kinyume cha sheria ya kanuni ya adhabu chini ya vifungu 332 na 337.

Katika shitaka la tano, alidai kuwa, Mchungaji Rwehumbiza akiwa kwa Kamanda Rwambow, Agosti 6 mwaka huu saa 7.45 mchana alitoa barua iliyoonyesha kuwa iliandikwa na Mwenyekiti wa DP Taifa ikimtambulisha wadhifa huo wa mwenyekiti wa chama wa mkoa.

Mtikila pia anadaiwa kutoa barua ya uongo kwa kamanda Rwambow.

Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi, Janet Masesa ndiye anayesikiliza kesi hiyo.

Baada ya watuhumiwa wote kutoa maelezo yao jana, wakiwa na mtetezi wao Steven Magoiga waliwasilisha ombi la dhamana kwa Hakimu Masesa, alilikubali.

Aliwataka wawe na wadhamini wawili kwa kila mtuhumiwa. Walipatiwa dhamana ya kauli ya Sh.500,000 kwa kila mmoja sanjari na kutoa barua za dhamana. Kesi iliahirishwa hadi Septemba 10 mwaka huu.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la habari leo;07/08/2009
 
Huyu wamfunge tu maana anacheza na mungu....
 

Dhambi ya ufisadi lzm itakugeuka na kukula unayeitenda;baada ya kumfanyia kazi nzuri EL na RA ya kumchafua sana mzee Sumaye na baadae Mzee Dr Salim leo hawana haja nae tena mchungaji Mtikila!

Niliposoma tu kuwa yupo Mwanza anawaelekeza wananchi huko ubaya wa CCM nikajua his days uraiani is numbered!mnafiki wewe sina huruma hata chembe na wewe kwa kuharibu upinzani TZ hasa ulipotumwa kule Tarime!

Labda utoke jela kwa dhamana ukitumia baadhi ya milion 3 alizokupa RA kama asante ya kutuvuruga!shame on you!

"Mtikila what you did for us previously is what you get today"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…