Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,762
- 59,204
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Mtikila kutinga kortini posho za wabunge[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Thursday, 02 February 2012 21:32[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
KITENDO cha wabunge kujiongezea posho kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 bila idhini ya Rais, kimemkera mwenyekiti wa Chama Cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila ambaye sasa amesema anajiandaa kwenda mahakamani kufungua kesi ya kughushi dhidi ya viongozi wa taasisi hiyo ya kutunga sheria.
Mtikila aliliambia gazeti hili jana kuwa kama kweli Rais Kikwete hajasaini posho hizo, basi bunge limeghushi na kuliibia taifa na kitendo hicho hakiwezi kuvumilika.
Alisema tayari ameanza maandalizi ya kesi hiyo kwa kuwatafuta wanasheria wa ndani na nje ya nchi watakaosimamia mahakamani hadi haki itakapotendeka.
Alisema mshtakiwa namba moja katika kesi hiyo ni Spika wa Bunge Anne Makinda, wa pili ni naibu wake Job Ndugai na baadaye wabunge wote wanaosaini nyongeza hiyo ya posho isiyokuwa na baraka za rais.
"Huku ni kughushi na kuhujumu uchumi wa nchi, Bunge kujiongezea posho bila idhini ya rais! ni wizi wa kawaida kabisa ambao ni kosa la jinai. Niko mbioni kukamilisha taratibu na hakika ninaenda mahakamani," alisena Mtikila.
Kwa mujibu wa Mtikila, mbali na Bunge kesi hiyo pia itamhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
"Yeye atahusika kwa sababu ameliona hilo na ameendelea kukaa kimya. Huu ni uzembe na sheria zinasema kutenda au kutotenda kunakoleta madhara ni kosa."
Mtikila alisema anasikitika kuona viongozi waliopewa fursa ya kuwatumikia wananchi, wanatumia fursa hiyo kuwajumu na hii haivumiliki.
Nitaenda mahakamani kwa sababu hili suala sio la mchezo kabisa linaumiza wananchi, alisema.
Hata hivyo Mtikila hakusema lini atafungua kesi hiyo zaidi ya kusisitiza kuwa bado anaendelea na maandalizi ya kutafuta wanasheria.
Mtikila alieleza kuwa matatizo yanayolikabili taifa kama hili la wabunge kujiongezea posho kinyemela, linatokana na matatizo ya katiba ambayo watanzania wanapaswa kujipanga kuyaondoa katika mchakato huu wa katiba mpy[/TD]

0digg
Hussein Issa,