Mtikila kutinga kortini posho za wabunge

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
54,762
Reaction score
59,204
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Mtikila kutinga kortini posho za wabunge[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Thursday, 02 February 2012 21:32[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
0digg
Hussein Issa,
KITENDO cha wabunge kujiongezea posho kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 bila idhini ya Rais, kimemkera mwenyekiti wa Chama Cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila ambaye sasa amesema anajiandaa kwenda mahakamani kufungua kesi ya kughushi dhidi ya viongozi wa taasisi hiyo ya kutunga sheria.

Mtikila aliliambia gazeti hili jana kuwa kama kweli Rais Kikwete hajasaini posho hizo, basi bunge limeghushi na kuliibia taifa na kitendo hicho hakiwezi kuvumilika.

Alisema tayari ameanza maandalizi ya kesi hiyo kwa kuwatafuta wanasheria wa ndani na nje ya nchi watakaosimamia mahakamani hadi haki itakapotendeka.

Alisema mshtakiwa namba moja katika kesi hiyo ni Spika wa Bunge Anne Makinda, wa pili ni naibu wake Job Ndugai na baadaye wabunge wote wanaosaini nyongeza hiyo ya posho isiyokuwa na baraka za rais.

"Huku ni kughushi na kuhujumu uchumi wa nchi, Bunge kujiongezea posho bila idhini ya rais! ni wizi wa kawaida kabisa ambao ni kosa la jinai. Niko mbioni kukamilisha taratibu na hakika ninaenda mahakamani," alisena Mtikila.
Kwa mujibu wa Mtikila, mbali na Bunge kesi hiyo pia itamhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

"Yeye atahusika kwa sababu ameliona hilo na ameendelea kukaa kimya. Huu ni uzembe na sheria zinasema kutenda au kutotenda kunakoleta madhara ni kosa."

Mtikila alisema anasikitika kuona viongozi waliopewa fursa ya kuwatumikia wananchi, wanatumia fursa hiyo kuwajumu na hii haivumiliki.

“Nitaenda mahakamani kwa sababu hili suala sio la mchezo kabisa linaumiza wananchi,” alisema.
Hata hivyo Mtikila hakusema lini atafungua kesi hiyo zaidi ya kusisitiza kuwa bado anaendelea na maandalizi ya kutafuta wanasheria.

Mtikila alieleza kuwa matatizo yanayolikabili taifa kama hili la wabunge kujiongezea posho kinyemela, linatokana na matatizo ya katiba ambayo watanzania wanapaswa kujipanga kuyaondoa katika mchakato huu wa katiba mpy[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Alisema mshtakiwa namba moja katika kesi hiyo ni Spika wa Bunge Anne Makinda, wa pili ni naibu wake Job Ndugai na baadaye wabunge wote wanaosaini nyongeza hiyo ya posho isiyokuwa na baraka za rais.
kama vipi pitisha ata bakuli tukuchhangiwe ili uwaburuze japo hutashinda kesi
 
Me namshauri aziangalie na achukue salary slip za wabunge hili iwe ushahidi mahakani si mnajua viongozi wetu vigeugeu wasije wakamgeuka kwamba posho raisi ajazibariki
 
Me namshauri aziangalie na achukue salary slip za wabunge hili iwe ushahidi mahakani si mnajua viongozi wetu vigeugeu wasije wakamgeuka kwamba posho raisi ajazibariki
mawakili watalifania kazi hili
 
Kuna zile kesi za mgombea binafsi alisema anafungua upya zimeishia wapi? Asisahau kufungua na ile ya kudai Tanganyika yetu
 
Ukiona hivyo ujue amesha CHACHA hapo anatafuta hela za kumziba domo, Akishahongwa tu anatulia tuliiiii humsikii tena mpaka achache tena
 
Bora Mtikila aende atusaide kutusemea-maana kwa nchi hii ni yeye tu mwenye guts za kwenda mahakamani na kushtaki serikali
 
Mtikila sasa anahitaji support yetu!! Yeye mahakamani, sisi barabarani!!
 
Sorry if I'm being too offending....

Hivi mtikila ana akili timamu kweli?

Si maanishi kwamba hajui anachokifanya ila kuna aina Fulani ya ukichaa huwa baadhi yetu tunao ni mania type of psych... Hivi sasa hebu wataalam tusaidianeni hapa

Kuna sex mania,etc etc

Hebu mtujuze kila nikihisi , nikidhani , nikidadavua ,nikikokotoa na nikicalculate napata mkorogano Kidogo kuhusu huyu mtikila...

Nawasilisha.
 
Siku CCM wakiachishwa ngazi, natamani Mtikila ndo awe mwanashiria wa serikali, ili asaidiane na waziri wa sheria kurekebisha uozo wa serikali ya CCM nchi iwe safi
 
huyu mchungaji apewe hata uzee wa baraza kwa kushinda mahakamani inaonekana ana mzio na sebule yake ndio maana anashinda kwenye mabenchi mahakamani
 
Nilikuwa nimemisi pilika za kesi zake..juzijuzi nimemuona amepanda bajaji hapo posta, sijui yake au alikuwa kakodi
 
Kortini akuna haki dawa yao ni kuhandamana tu. HIPO SIKU UTAJISHITAKI MWENYEWE Mchungaji
 

bla shaka wewe unahitajika upelekwe milembe ukapimwe akili. Mtikila hana tatizo lolote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…