Mtikila kutinga kortini posho za wabunge

Wazo zuri sana ila mahakama haitatoa haki maana serikali imejikita humo......
 
Hapo ndipo anaponikosha Mtikila, alijifuza kuwa kuingia mitaani hakuna tija unaishia kula mkong'oto na kulala rumande.

Hivyo ndivo inavyotakiwa, hata ukidhulumiwa record zitakuwepo na vizazi na vizazi watazikuta na kujifunza.
 
hili jamaa sometimez lina akili....hii ilitakiwa kufanya na chama "kikuu cha upinzani" lakini bahati mbaya nacho kimelewa ulevi wa posho kwa kuwa kuna watu wa zito wa chama hicho wananufaika na kilevi hicho,sasa wako tila lila mpaka miwani inadondoka hawaoni tena au wanaona kwa makengeza!
 
Bora Mtikila aende atusaide kutusemea-maana kwa nchi hii ni yeye tu mwenye guts za kwenda mahakamani na kushtaki serikali

Tunawaomba wabunge wote waliokuwa wanazipinga hizo posho wamsaidie mtikila kwa kumpatia data zote nasi watanzania tuwe pamoja kumwunga mkono mchungaji wa Mali za watanzania aliyejitokeza kufungua mashitaka kwa wale wote waliohusika kuizinisha hizo posho kinyemela.hongera sana mtikira.
 
Tatizo letu watanzania wengi hawajauelewa mchango wa Rev. Mtikila katika kuleta demokrasia Tanzania.

Ni Mtu anayefungua kesi sio kwa mnufaa yake Bali kwa manufaa ya watanzania wote. Mtu yoyote anayebeza juhudi zake katika Nyanja ya sheria basi atakuwa na upungufu wa busara kichwani.

Akifungua kesi asisahahu kufungua na kesi nyingine kuishtaki serikali kwa kupuuzia Madai ya madaktari kitendo kilichosababisha mamia ya watanzania kufa katokana na kukosa huduma za afya. Haki ya kuishi inayoelezwa kwenye Katiba ni pamoja na haki ya kupata matibabu ya kutosha ya bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…