RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 55,727
- 123,094
Mtikila akusudia kuzuia Uchaguzi Mkuu
Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Chritopher Mtikila, ameungana na azma ya Chama Cha Jamii (CCJ), kutangaza kusudio la kuiomba Mahakama Kuu isimamishe Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Tofauti na CCJ inayoazimia kuzuia uchaguzi huo iwapo ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, haitatoa usajili wa kudumu kabla ya kuanza kwa mchakato wake (uchaguzi), Mchungaji Mtikila, anaainisha sababu mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mchungaji Mtikila, alitaja sababu hizo kuwa ni marekebisho ya kifungu cha Sheria ya Uchaguzi kinachozuia matokeo ya mgombea urais kuhojiwa na chombo chochote baada ya kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mchungaji Mtikila, alisema kifungu hicho kinapaswa kufutwa ili kukidhi matakwa ya haki za binadamu na misingi ya demokrasia.
Mchungaji Mtikila alitaja sababu nyingine kuwa ni kutoa fursa kwa mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura, aruhusiwe hata kama hana kitambulisho cha mpiga kura.
Pia Mchungaji Mtikila, alitoa rai kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, kuharakisha hukumu ya rufaa ya kesi ya mgombea binafsi, ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea, kutokana na ucheleweshaji wa hukumu hiyo.
Alisema kitendo cha kutomtambua mtu asiyekuwa na kitambulisho cha kupigia kura na kumzuia kutochagua viongozi wake, ni kumnyima haki ya msingi.
Alitoa mfano kuwa sheria nchini Australia inatamka kuwa raia wake wenye sifa za kupiga kura wanastahili kufanya hivyo na kwamba ni kosa la jinai kuzuiwa kupiga kura.
Alisema sheria kama hiyo inapaswa kutumika hapa nchini ili wadau wa uchaguzi ikiwemo serikali, waelewe umuhimu wa kura za wananchi.
Alisema yapo mambo mengi katika Katiba ya nchi, ambayo yanatakiwa yabadilishwe ili Watanzania waweze kuwa na wigo mpana wa kufanya uamuzi kuhusu nchi na rasilimali, viwe mikononi mwao na vizazi vijavyo.
CHANZO: NIPASHE