Mtikila: Wameanza kutufunga ‘Luku’

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Mchungaji Christopher Mtikila, amewaacha hoi wajumbe wenzake pale alipotaka kanuni zisiwabane kuwasema vibaya waasisi wa Muungano.

Kanuni ya 47 ya rasimu za Bunge hilo, zinakataza mjumbe kutumia jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, kwa dhihaka au kwa lengo la kutaka kulishawishi Bunge.

Kanuni hiyo ilimfanya mjumbe wa Bunge hilo, Ezekiah Oluoch, kupendekeza wajumbe wazuiwe kuwasema vibaya marais hao na waasisi wa Muungano waingizwe katika kanuni hiyo.

Hoja hiyo ilionyesha kumgusa Mchungaji Mtikila ambaye alipinga hatua ya kuwazuia wajumbe kuwasema vibaya waasisi hao na kwamba binafsi anaona kama wajumbe wameanza kuwekewa Luku.

“Naona kama tumeanza kuwekewa Luku kwa suala nyeti kama la Muungano, kusema waasisi wasisemwe vibaya au isivyopendeza mimi naona siyo sawa,”alisema Mchungaji Mtikila na kuongeza;

“Naomba hilo liondolewe kabisa ili watu wawe huru kuzungumza juu ya watu wanaowawakilisha kwa mamilioni hapa ndani kwa kufanya hivyo, tutaumia vizuri uhuru wa kujieleza”.

Akijibu hoja hiyo, mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kanuni, Evod Mmanda alisema, kuingiza majina ya waasisi ni jambo lisilowezekana kwa sababu idadi na majina yao hayajulikani.
 
Mtikila anatafita sababu ya kumtukana Nyerere.
 
Tusiwe na mawazo mbonyeo, kama kuna makosa yalifanywa na waasisi lazima tuseme. Mawazo ya waasisi sio Msahafu wala Biblia, na wala hawakuwa MTUME au YESU.
 
Kuna watu ukitaja jina Nyerere basi wanatetemeka maungo yao yote utadhani limetajwa jina la Mungu vile...

Ndio maana kushughulikia kero za muungano na muundo mpya wa muungano inakuwa vigumu..
 
Hatuwezi kukumbatia mawazo ya waasisi hata kama hayako sahii eti kisa tunalinda legacy zao, hapana lazima mabaya wajadiliwe pia, mbna nyerere ali admit kuwa katika awamu ya kwanza kuna mazuri na mabaya hivyo akatuasa tuache mabaya na tufuate mazuri, sasa tutachambuaje mazuri na mabaya yao bila kuwajadili?
 
Kumbe shida ni kuwasema vibaya, kwahiyo waangalie wenyewe namna ya kuwasema bila kusema vibaya.
 
Mbona kipengele kinajieleza? "Majina hayo yasitumiwe kwa dhihaka"! Maana yake hajakatazwa mtu kuyatumia ila asiyadhihaki. Sioni mantiki ya kutaka kukipinga, au wanaotetea kitoke wanataka kuendeleza lugha chafu tulizozisikia huko? Labda hoja ya msingi yangeomba tafsiri ya dhihaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…