MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 785
MWENYEKITI wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, amekiri kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa ni mpambanaji wa siasa za mageuzi na anastahili kuungwa mkono na Watanzania.
Mtikila alieleza hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Chacha Wangwe kilichotungwa na Mwanaharakati Deo Meck.
Alisema akiwa bungeni Dk. Slaa aliweza kupambana na hata kurekebisha yale ambayo serikali kwa makusudi iliyaficha kwa maslahi yake na kuwataka Watanzania kuwapima wagombea kutokana na sifa na vigezo vyao.
Akizungumzia marehemu Wangwe alisema: Kifo cha Chacha Wangwe kimetufundisha mengi na tunahitaji kuyaendeleza yale mazuri kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho; ni muhimu sasa tuyafanye kwa maslahi ya taifa letu, alisema Mtikila.
Aidha, alisema kitabu hicho kitasaidia kuleta siasa za kweli kwa kufanya yale ambayo marehemu Chacha Wangwe aliyafanya akiwa bungeni kwa maslahi ya Watanzania na kuwatetea wanyonge.
Kwa upande wake mtunzi wa kitabu hicho, alisema kitabu hicho amekitunga kwa nia ya kukumbuka yale mema aliyoyafanya marehemu Wangwe na sio kumsema mtu kama ilivyodhaniwa na baadhi ya watu.
Leo ninazindua kitabu hiki kwa maslahi ya kumbukumbu zetu wala sina chuki na mtu yeyote na wala sijamsema mtu wala taasisi yoyote, Watanzania wakisome wachukue yaliyo mema hasa hasa aliyoyafanya Wangwe, alisema Deo.