Mtikilia adai kutojiunga na mtandao wa "Saidia Kikwete Ashinde"!

Nahisi kuna ukweli fulani katika madai ya Mtikila kwani ni mazito sana. Nitashangaa kama hatachukuliwa hatua.
 
Mimi naamini kabisa kuwa JK anaweza kabisa kumtumia huyu jamaa.Mtikila ni chizi nayefanya kazi na mtu yeyote ili mradi tu mkono uende kinywani.
 
Mimi naamini kabisa kuwa JK anaweza kabisa kumtumia huyu jamaa.Mtikila ni chizi nayefanya kazi na mtu yeyote ili mradi tu mkono uende kinywani.
kwani amewahi kupimwa akili yake huyu mjamaa wa kutoka NJOMBE.
 

Ur right Kiranga.

Hayo mambo ambayo Mtikila ameambiwa ayafanye/aseme ndiyo hayo hayo yanayosemwa na viongozi wa baadhi ya vile vyama vichache dhaifu (Lifa Chipaka, Mrema). Leaders of small & weak opposition parties are the targets here. Yaelekea hao wanaoropoka (Chipaka, Mrema) walikubali hayo maelekezo.

Yaonekana hii ni pattern ambayo imeanza, kuwa wanaambiwa:
1. Wanaelekezwa washutumu kauli za mkutano ulioitishwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (zile kauli za kukosoa tu).
2. Wanaambiwa waunge mkono 'utabiri' wa Sheikh Yahya kuwa yeyote atakayejitokeza kugombea urais kwa tiketi ya CCM (ukiacha Kikwete) atakufa ghafla. (Au atauawa?)
3. Wanaelekezwa kumshutumu yeyote atakayemkosoa Rais Kikwete siku za baadaye.

Du, yaelekea huyu jamaa hataki kukosolewa kabisa. Ndio maana anafanya mambo ya ajabu kabisa utadhani hana washauri. Urais ni taasisi, hata Rais akitaka kuharibu, ni jukumu la washauri kumshauri, ila yaelekea hawasikilizi na hatimaye wanaacha/wanaogopa kumshauri, wanabaki kukubaliana naye tu lolote analotaka).

Pity Tanzania...
 
Na kisha imekwishanenwa...atakayempinga atafariki ghafla!
 
What is real happening within CCM? why are these primitive things happening now 2010 not during 2005 or 2000 elections? nafikiri kuna tatizo ndani ya CCM hawataki tu kusema kuna kale ka hali ka kutojiamini hasa kwa mgombea wao. Kikwete ni yule yule wa 2005 hatukusikia CCM wanababaika kiasi hiki mara watabiri mara kupinga taasisi ya mwl Nyerere mara saidia Kikwete asinde utadhani taifa staas something is wrong somewhere within CCM yenyewe wait and see.
 
mimi binafsi sioni kosa la mtikila, yeye alikuwa anaeleza maoni yake binafsi, hasa akizingatia nchi hii ni ya kidemokrasia. hapa napata hofu sana, na zaidi sana kwenye kesi hii mkono wa raisi na hakika upo, kwa sababu raisi anafahamu kuna kesi ya namna hii, kama angekuwa kinyume nayo angeisimamisha. kama alivyoweza kuingilia kesi ya br. dito na wengine wengi aliyo wasaidia km kina rostam. hii kesi inaonyesha kwa kiasi gani raisi hataki kukosolewa, hivyo kuonyesha kiwango chake kidogo cha kujiamini na utendaji.

mwisho. lawama zangu zote zinaenda kwa wandishi wa habari badala ya kuonyesha nchi hii hakuna demokrasia wanatuonyesha namna gani mtikila hafai. hapa kikwete ndio hafai badala ya kuendesha nchi kidemokrasia anaiendesha nchi kibabe,mtu asiseme lolote kuhusu raisi kwani waandishi badala ya kuonyesha kikwete hafai wanatuambia mawaziri wa kikwete wameoza, wataoza vipi wao kabla ya kikwete. waandishi acheni kuzunguka mbuyu muwe wakweli. fimbo inayo muuwa nyoka yaweza kumuwa binadamu.
 

Gosheni,
Kwa kuongezea, wengi wa mawaziri ambao wanaonekana kushindwa kutekeleza majukumu yao ni wale walio karibu zaidi na Rais, Lowassa & Rostam (mawaziri hawa wanajulikana zaidi kama washkaji, na inaaminika kuwa wamepata madaraka kutokana na ukaribu wao na hao watu watatu).

WaTZ wana tabia ya kuzunguka, na hii tabia inatakiwa ife. Itamkwe tu Kikwete na baadhi ya mawaziri wake wameshindwa kutekeleza majukumu yao. nao watajwe. na mawaziri waliojitahidi na kufanya mazuri watajwe. Kikwete hata ukumkosoa kishkaji tu na kupuliza anakasirika, afadhali umkosoe kiukweli kabisa.

Dito alionekana kuua makusudi, akabadilishiwa mashtaka ili apate dhamana.

Ingekuwa Tanzania ni nchi yenye taasisi huru (Strong & independent institutions) kama ilivyo kwa mfano Marekani haya matamshi ya Mtikila yangefanyiwa uchunguzi, na wenye hatia wangechukuliwa hatua.

Hapo zamani Marekani uchunguzi huru ulisababisha Rais Richard Nixon na Makamu wake wakajizulu (Nixon aliwahi kujiuzulu akiepuka Bunge kumpigia kura ya kumfukuza kazi ya Urais).

Theoretically, hata Bunge la Tanzania linaweza kuunda Tume Huru kuchunguza madai ya Mtikila.
 
kwani ukishindwa kujiheshimu,ama kutekeleza masharti ya dhamana wakati ukiwa na kesi unastahili kufanywa nini??sitaki amini sheria hazipo wazi kwenye hili na wala siamini kuna wanaotaka Mtikila awe juu ya sheria sababu ame'mention kukataa 'kununuliwa' na katibu wa rais..haya mambo mengine bana,si angeitisha mkutano na waandishi wa habari akamsemea katibu wa rais kwa watanzania wakati huo?nini kilimzuia?ama alikuwa 'anajifikiria' kama airudie ofa 'aendeleze familia yake'?kwa nini aseme alikataa kujiunga na huo mtamdao wakati amebanwa na sheria kwenye makosa yake mengine,sympathy seeker...
 
Huyu mchungaji lazima utumie akili ya ziada kama unataka kuziamini kauli zake. nyingi zina utata...
 
Hapa sasa Mh. Rais atashindwa pa kuanzia.

Ndo maana kuna vijiswali huwa namuuliza kama mpiga kura hajanijibu mpaka leo wakati na yeye ni mwana JF mzuri tu hata kama ni Guest ile kusoma tu inatosha. Jiunge basi unijibu mzee.

Ukijibu maswali ya wapiga kura huhitaji kugharimika bure na hiyo mitandao ambayo baadaye inataka fadhila.

Ebu jibu maswali yafuatayo

1. Kwa mujibu wa ahadi zako 2005 mahakama ya kadhi ilitakiwa iwe imeshaanza mpaka sasa......iko wapi? Kama unataka kuchaguliwa 2010 ni lazima uamue moja mapema....acha kudanganya waislamu kwa kuwaonyesha nyaraka feki kwamba suala liko mbioni wakati unajua kabisa vatican wamekunyooshea ngumi. Au unataka kujihalalishia miaka mingine mitano...kwani ahadi yako ilikuwa kwa kipindi cha miaka kumi???...sasa Gharama za uchaguzi 2010 ni za nini?

2. Mafisadi wamechukuliwa hatua gani? unasingizia mahakama kama ilivyokuwa kwa Zombe? Kwa hiyo Huduma ya Siri hawana data kabisa wakati nchi inaendelea kutafunwa. Au wewe nawe ni fisadi?

3. TANESCO Imekushinda? TRL je? ATCL?

4. Udini na ukabila nchini mbona umezidi sasa?

5. Chama ambacho wewe ni mwenyekiti wake maendeleo yake yakoje? Je ni sawa na waliokutangulia? Na Katibu wa Chama uliyemchagua ni sawa na aliyekuwepo kabla? Anaimarisha au anabomoa chama? Mbona ni kama mnajenga CHADEMA na kubomoa CCM basi kwa nini msijiunge CHADEMA moja kwa moja?

6. Kati yako wewe na watu kama John Magufuli, Dr. Slaa, Dr Salim Ahmed, Prof Lipumba, Dr Ali Shein, Sumaye, Prof Tibaijuka na Shibuda nani anaweza kuwa Rais bora kwa 2010. Moyo wako unasemaje? Unawaweza hawa jamaa kikazi kweli?

7. Kati ya katibu wako wa chama Makamba na aliyekuwepo Mang'ula unaonaje kazi zao yupi anajenga CCM na yupi anabomoa na kujenga CHADEMA? Yupi ni mlea ufisadi?

8. Hivi Nyerere angefufuka leo si angekufa tena kwa mshtuko? Hivi ndivyo alivyokuacha humu duniani.....ebu nijibu umelishwa nini ukabadilika hivyo? mbona umepoteza msimamo? Uzalendo wako umeenda wapi? Inawezekanaje mtu asiyekuwa fisadi akalea mafisadi mbona hueleweki? umeanza woga lini soldier?

9. Huyu Kasim ni wewe ulimtuma kwa Mtikila? Kwa hiyo umewadharau watanzania na kuheshimu mitandao zaidi?


10.Miaka mitano ya kwako Kikwete, na miaka mitano ya kwanza ya mkapa ipi bora?

SIJUI WATAFUNGWA WANGAPI MWAKA HUU??????????DUH NAOGOPA SELO???????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…