Mtindo huu wa uezekaji unachangamoto gani?

TCSPM

Member
Joined
Dec 3, 2020
Posts
52
Reaction score
78
Habari!

Wana Jf Nina boma langu style hii inayoonekana pichani naipenda sana kwani haijaingia sana mtaani hasa maeneo niliosimika boma langu af pia kutokana na kipato changu 200k naona nitampuguza gharama nyingi hofu yangu sijui kesho ya hili nililo chagua mnaojua changamoto za style hii nijuzeni

 
Mbona iko poa tu mkuu. Cha msingi tu uwe umeipenda na umpate fundi wako makini.
 
Hii naona na gharama za kuezeka zitakuwa nafuu zaidi
 
Kule kijijini kwetu nimekuwa tangu nikowa mtoto nyumba kama hizo naziona na zimejengwa kwa matofauli ya kuchoma na udongo wa kawaida tu na zimedumj hadi leo.
 
Sijui Ni kwanini lkn napenda Sana roof ya zege kuliko kigae/bati.
 
Kwanza tofali unatakiwa ulaze ili ziweze kuhimili mzigo utakaokuja juu pia usiwe mbahili kwenye kanuni za zege yaani Nondo ziwe imara ratio nayo iwe nzuri
 
Kwan ni ghorofa?
Hata km ni Nyumba ya chini km juu unataka kuweka mzigo mkubwa inabidi msingi uwe imara kuepuka crackers ambayo inaweza pelekea zege la juu nalo kutengeneza njia za maji kuvujia ndani
 
Hata km ni Nyumba ya chini km juu unataka kuweka mzigo mkubwa inabidi msingi uwe imara kuepuka crackers ambayo inaweza pelekea zege la juu nalo kutengeneza njia za maji kuvujia ndani
Ok jee kama anaweka bati?
Hata kama anaweka zege kwann asiweke nguzo tuu?
 
Nyumba ndogo ila imetulia.
 
Hivi ukiezekea kwa bati mtindo wa slope nyumba hata kubwa kuna ubaya gani? Mana naona kama vile huku Tanzania tuna-gumuisha mambo sana.

Naona slope inapunguza gharama za bati + mbao. Kikubwa jengo unalipandisha juu tu!
 
Hizi zilikuwepo sana zamani kwa style ya slope, lkn hivi karibuni zimerudi kwa kasi zikiwa modified na kuwa na paa ndefu. Kwa ujumla zinapunguza gharama ya mbao na bati kwenye upauaji, lakini hapo unatakiwa kupata fundi specialist anayejua kupau vizuri. Asipoweka vizuri drainage system ya kukusanya na kutoa maji kwenye kona kila baada ya ya miaka 3 utakuwa unarekebisha paa sababu ya kuvuja
 
Inategemea jengo na jengo
Sio kila jengo linafaaa kuezeka hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…