Mtindo wa kusafirisha hela nyingi unapitwa na wakati

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Kwa wana Jf,

Leo nilikuwa nje ya Bank Moja ya Biashara nika bahatika kushuhudia mahela mengi yakisafirishwa. Pale kulikuwa na polisi (vijana) wawili wa umri kati ya miaka 25 na 30 hivi; ukweli niliwapenda kwani walikuwa makini sana na silaha zao nafikiri SMG lile sanduku la hela lilipokuwa lina pelekwa kwenye gari.

Kwa umakini kabisa walihakikisha limewekwa mahali husika, na kufungiwa kabisa kwa lock maalum. Wakaingia ndani ya gari (hilo lenye hela na kuanza safari)

Kwa mtazamo wangu;


  • Nahisi lile gari lenye hela lingeweza kwenda na driver peke yake au driver na mtu mmoja mwenye silaha ndogo (ya mkononi) halafu wale Askari walifuate kwa nyuma; ingekuwa ni salama zaidi.
  • Nahisi sasa imefika wakati wa kufanya ulinzi wa hela nyingi kwa kuzifuatilia kwa Pikipiki ambazo zitakuwa zinafuata kwa umbali fulani hivi na ziwe na namba za kawaida na wanaoziendesha wasivae Uniform.
  • Kwa mahela mengi sana (kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine ningependekeza zitumike helcopter au zisindikizwe na gari ambayo ni bullet proof na sio askari kukaa ndani ya gari na mahela kwani hiyo sio sawa kabisa.

Kwa ushauri wangu;


1. 1. Nafikiri sasa imefika wakati kwa Waajiri kushawishi wafanyakazi wafungue Akaunti kwenye benki zilizopo karibu na walipo ili wawe na utaratibu wa kulipa kupitia bank au hata cheque. Hiyo ni salama na huwezesha wafanyakazi kuwa na mazoea ya kutumia Bank na hivyo kuwa na matumizi mazuri ya hela zao.

2. 2. Kwa Sasa kuna huduma za Mpesa, Airtel Money, Tigo Pesa na wengineo; Wafanyakazi wa muda (vibarua) wanaweza kulipwa kwa huduma hizo; hii itawezekana kwa kampuni kuingia mkataba na wakala mkumbwa wa huduma hizo na hivyo kuwalipa wafanyakazi husika kupitia simu zao.

Nahisi kupitia mapendekezo haya, tutapunguza kusafirisha hela nyingi ambapo sio salama; kwani huleta usumbufu mkubwa kwa waajiri na waajiriwa bila kusahau usalama wa wasafirishaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…