Godfrey- denis
New Member
- Aug 26, 2022
- 2
- 4
MTINDO WA MAISHA YAKO NDIYO AFYA YAKO
Habari wanajukwaa ,mimi kama kijana wa kitanzania mwenye uchu wa mapinduzi chanya ya kiafya kwa watanzania nawaletea kwenu ujumbe huu unaogusia zaidi “Mitindo yetu ya maisha na mchango wake katika afya zetu”
UTANGULIZI
Kumekuwa na changamoto nyingi ambazo tumekuwa tikijaribu kuzitatua katika Nyanja ya afya ndani ya nchi zetu za kiafrika na dunia nzima.Changamoto hizo ikiwa ni kama hali mbaya ya kiuchumi,elimu,uhaba wa vifaa tiba,uhaba wa wahudumu wa afya,majanga ya asili, na uhaba wa viytuo vya afya. Lakini mbali na changamoto hizo tumesahau kuwa mitindo yetu ya maisha ndiyo changamoto kubwa katika afya zetu. Basi kutokana na changamoto hiyo katika Makala hii nitaelezea baadhi ya mitindo mibaya ya maisha na athari zake katika maisha yetu.
HALI HALISI YA KIAFYA KWA SASA
Ndugu zangu katika wakati wa milipuko mbalimbali ya magonjwa hatari yanyoikumba dunia, kama UVICO -19, Homa ya nyani na EBOLA hali ya kiafya kwa ujumla sio nzuri sanjari na kudorora kwa hali za kiuchumi. Mbali na magonjwa hayo kuna magonjywa mengine mengi kama magonjwa ya moyo,magonjwa ya mapafu,magonywa figo,ngozi na uzazi bila kusahau magonjwa ya saratani ambayo kwa asilimia kubwa yanasababishwa na mitindo yetu mibaya ya maisha.
Ifuatayo ni mitindo mibaya ya maisha na madhara yake katika afya zetu:-
1.UVUTAJI WA SIGARA NA MADAWA YA KULEVYA.
Uvutaji wa sigara ni moja ya mitindo mibaya katika maisha yetu, ambayo ufanywa kwa asilimia kubwa na vijana ambao ndo nguzo kubwa ya taifa.
Madhara ya uvutaji wa sigara na matumizi ya kulevya ni kama ifuatavyo:-
Husababisha magonjwa ya upumuaji: Hii hutokana na kemikali kutoka kwa moshi wa sigara na tumbaku ambazo husababisha kuongezeka kwa magonjwa ya mapafu ambayo kwa ujumla huitwa COPD(Chronic Obstructive Pulimonary Diseases) .
Huchochea utokeaji wa magonjwa ya akili.Uvutaji wa sigara na matumizi ya madawa ya kulevya huchangia asilimia 14% ya ugonjwa wa Alzheimer’s( ugonjwa wa udhaifu wa kiakili).
Ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya moyo na mifupa ambayo huitwa coronary heart diseases.
Uvutaji wa sigara na tumbaku kwa mama mjamzito huchangia kifo cha mama na mototo mchanga, lakini pia uvutaji wa sigara kabla ya ujauzito kunaweza kupunguza uwezo wa kuzaa.
Uvutaji wa sigara huathiri mtiririko wa damu na mishipa ya damu vyote hivi uchangia matatizo ya uume na uwezo wa kuzaa.
Uvutaji wa sigara huchangia ugonjwa wa Arthritis ambao husababisha kifo cha mapema,ulemavu, na kudhoofisha ubora wamaisha.
Hayo tu ni machache kuhusu uvutaji wa sigara,utumiaji wa madawa ya kulevya na madhara yake.
SOURCE: Verywell Mind
2.UNYWAJI WA POMBE KUPITA KIASI
Unywaji wa pombe kupita kiasi huambatana na madhara mengi sana katika afya zetu.Baadhi husababishwa moja kwa moja na pombe mengine huchochewa na unywaji wa pombe kupitiliza. Yafuatayo ni madhara ya unywaji wa pombe kupita kiasi :-
Unywaji wa pombe kwa madereva wengi husababisha ajali za barabarani ambapo matokeo yake ni kupoteza maisha na kupata ulemavu wa kudumu.
Matumizi ya pombe kupita kiasi kwa mama wajawazito husababisha vifo vya vichanga.
Unywaji wa pombe kupita kiasi ukiambatana na ukosefu wa vitamin A,B1 na B2 husababisha upungufu wa uwezo wa kuona.
Unywaji wa pombe kupita kiasi husababisha upotevu wa maji mengi mwilini.Hii ndo sababu walevi wengi hupata haja ndogo mara kwa mara wakilewa.
Kwa wanaume unywaji wa pombe kupita kiasi hupunguza uwezo wa kushiriki vyema tendo la ndoa.
Unywaji wa pombe kupita kiasi husababisha kushuka kwa kiasi cha sukari mwilini. Hii hutokana na madhara ya pombe kwenye kongosho ambayo huzalisha kiasi kikubwa cha insulin ambayo husababisha matumizi makubwa ya sukari mwilini.
Unywaji wa pombe kupita kiasi husababisha magonywa ya ini kwa namna tofauti.
Matumizi ya pombe kupita kiasi hasa kwa wanawake huwaweka katyika hatari ya kupata saratani ya maziwa.
Hayo pia ni machache kwa upande wa matumizi ya pombe kupita kiasi.
Source: Michael’s house
3.UZEMBE NA KUTOKUFANYA MAZOEZI
Kukaa bila kazi au kutofanya mazoezi ya viungo vya mwili huambantana na mtokeo mabaya kiafya kama ilivyohainishwa hapo chini:-
Uzembe huambatana na uzito uliopitiliza ambao hutuweka katika hatari ya kupata magonjwa kama shinikizo la juu la damu, kujikusanya kwa mafuta katika mishipa ya damu( atherosclerosis) na magonywa mengine mengi ya moyo.
Lakini pia mrundikano wa sumu mwilini kama ammonia hutokea kutokana na ukweli kuwa ufanyaji wa mazoezi hupunguza mrundikano wa sumu mwilini.
Kutokufanya mazoezi husababisha mzunguko mdogo wa damu,ambao husababisha sehemu muhimu za mwili kukosa damu ya kutosha.
Hayo ni mchache tu yatokanayo na kutokufanya mazoezi ya mwili
Source: University of Nebrasca
4.ULAJI MBOVU.
Ulaji mbovu ni chanzo kikubwa cha magonjwa mengi katika afya zetu.Asilimia kubwa huwa tunakula bila kufata utaratibu mzuri wa lishe bora.Jambo hili husababisha madhra makubwa katika afya zetu kama ilivyohainishwa hapo chini:-
Ulaji wa chumvi kupita kiasi husababisha shinikizo la juu la damu.
Unywaji mdogo wa maji husababisha upungufu mkubwa wa maji mwilini ambao huambatana na kiasi kidogo sana cha damu mwilini.Lakini pia husababisha choo kigumu.
Ulaji mdogo sana wa matunda husababisha upungufu mkubwa wa kinga mwilini.
Ulaji wa mafuta uliopitiliza husababisha shinikizo la juu la damu na magonjwa ya moyo.
Ulaji mdogo wa mboga za majani husababisha upungufu wa madini ya chuma amabayo ni muhimu sana katika utegenezaji wa damu, lakini pia ukosefu wa mboga za majani husababisha kuwa na choo kigumu.
Hayo pia ni machache kati ya mengi yanayotokana na ulaji mbovu.
Source: Medical tips
5. UTUMIAJI WA VIFAA KIELECTRONIKI KWA MDA MREFU.
Mbali na kuwa matumizi ya vifaa vya kielectroniki kama; simu za mkononi na kompyuta mpakato ni muhimu katika mapinduzi haya ya teknologia, yapo madhara mengi yanayoambatana na matumizi ya vifaa hivyo kwa mda mrefu. Kwa mfano matumizi ya simu za mkononi kwenye mwanga hafifu huweza
kusababisha uono mbovu.
NINI KIFANYIKE?
Yafuatayo yanaweza kusaidia kuondoa changamoto hii:-
Kuhamasisha na kutoaelimu juu ya ulaji sahihi wa mlo kamili.
Kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya na matumizi ya sigara.
Kupiga vita matumizi mabaya ya pombe kupita kiasi.
Kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi ya mwili.
Kujali mazingira ya afya na mwili.
Kutoa elimu katika vyuo vya afya juu ya mchango wa mtindo wa maisha katika afya zetu.
HITIMISHO
Ningependa kuhitimisha kwa kusema ‘Afya ni mtaji’ tuzilinde afya zetu
Imeandikwa na,
Ndg., GODFREY DENIS

Upvote
5