Mtizamo wangu kwa idara za kiusalama

Mtizamo wangu kwa idara za kiusalama

Izy_Name

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2020
Posts
772
Reaction score
1,733
Ningependa kutoa ushauri wangu juu ya tathmini fupi nilioifanya kwa macho na kwa kutafakari juu ya baadhi ya idara mbalimbali hapa nchini.

1. Nikianza na TISS ningependekeza kuwe na idara mbili zenye kufanya kazi sawa na TISS bila ya kuwa ushilikiano wa aina yeyote wa kiutendaji katika majukumu.

- Hii itasaidia kuongeza umaridadi katika utendaji wa kazi za kiupelelezi kati ya TISS na X kwani kutaongeza umahili kutokana na kuwa na ushindani wa kutafuta na kufukunyua majawabu mbalimbali.

- Itasaidia kupunguza mambo ya siasa katika hizi idara nahata kupunguza kabisa kuingiliana na wanasiasa kama ilivyo sasa sababu kuu itakuwa kuonesha umahili.

2. Jeshi la polisi kuna baadhi ya mambo naona hayako sawa.

- Kwa upande wa jeshi la polisi ile kanuni/sheria/utaratibu etc ya kwenda polisi bure kutoka pesa iondolewe au ifutwe maana hii ndiyo chanzo cha kamatakamata hovyo mitaani (watu wanakamatwa bila hatia kumtoa kituoni mpaka pesa, kuna watu wamekaa selo kisa wamekosa ndugu wa kuwatolea TSH 10,000 tu) hii polisi wameifanya kama njia ya kujipatia kipato kwa njia za kionevu.

- Kama utaratibu huu utafutwa watu walioko selo na jail watapungua maana hamna polisi atakae ingia mtaani kukamata raia na wakati anajua hatapata kitu, na kesi za kubambikiwa zitapungua.

- Mdhamana iwekwe wazi na raia waelewe kuwa ni bure ili kupunguza utapeli wa polisi.

- Endapo mtuhumiwa ikibainika hana kosa aachiwa aondoke bila kulipa freely na ikibidi alipwe muda wake (Hii itahusu zaidi mahakani kama akitaka kufungua kesi ya kupotezewa muda + mateso ya polisi).

NB. Asilimia kubwa ya kesi nyingi za uzurulaji na uzembe ni uhuni wa polisi.

3. Mahakama iwe makao makuu inayofuatilia shughuli zote za mahakama nchi zote kwa real time.

- Kama mahakama zitakuwa na makao makuu inayofuatilia shughuli zote za mahakama nchi nzima hii itasaidia kupunguza rushwa na kunyimwa mdhamana bila sababu za msingi, kwa sababu hakutokuwa na uwezekano wa judge kupindisha sheria wakati anajua kuna
 
Katiba Mpya katiba Mpya.
Nje ya hapo mawazo yako mazuri hakuna atakayejali.
 
Idara ya TISS mfumo wake ni kama mfumo wa kimuundo na kiutendaji wa idara ya kijasusi ya Russia ya KGB wakati huo.

Kwa sababu kihistoria KGB imetokana na mfumo wa kisiasa wa kikomunisti uliotokea baada ya mapinduzi ya 1917.

Na mafunzo ya hawa makachero wa kwetu wengi wameyapatia huko Urusi au Cuba kwenye siasa za kikomunisti zilikozaliwa.

Kwahiyo sasa usishangae UVCCM ndio wapo enrolled kwa wingi huko, ni mfumo wa itikadi za chama.

Kwa hiyo idara lazima ikilinde Chama mama. Ingawaje wanasiasa kwa sasa wanaitumia hii idara kwa maslahi binafsi kwa asilimia kubwa. Na nadhani ikitokea CCM imedondoka leo au kesho, hii idara lazima itikisike kama sio kusambaratika.

Watu sometimes hujiunga na idara hii kwa maslahi mapana ya kuitumikia nchi yake kiuzalendo lakini mwisho wa siku akizama mfumoni inakuwa sasa anafanya kazi kwa maslahi fulani fulani ya viongozi.

Mfano kunyanyasa vyama vingine, kupoteza watu kimtindo ambao wako against the State. Na pia kufacilitate kwenye upigaji wa wanasiasa.

😂😂 Laiti kungekuwa na watu smart kama idara za CIA ambayo ipo independent kiutendaji na haiingiliwi kizembe na wanasiasa walafi.

Kwa mfano, CIA iliwahi kukumbwa na kashfa mbalimbali na mbaya zaidi ni ile kutumika kisiasa hususan kipindi cha utawala wa Richard Nixon na skendo ya Watergate. Tokea hapo wakajifunza.
 
Back
Top Bottom