DOKEZO Mto Goba unazama kwenye taka. Hii inaonekana hata kutoka angani

DOKEZO Mto Goba unazama kwenye taka. Hii inaonekana hata kutoka angani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Uchafuzi wa mto Goba unaweza kuonekana kutoka angani. Hamuamini? Angalieni picha zilizo chini. Zinaonyesha picha za satelaiti za mto Goba. Kati ya 2018 – 2021, kulikuwa hakuna maeneo makubwa ya kutupa taka. Lakini ukilinganisha picha hizo na za mwaka 2024, utaona kwamba pembezoni mwa mto kunatumika kama maeneo makubwa ya kutupia taka.

Ni tishio moja kwa moja kwa afya ya umma. Maji machafu, taka hatari kutoka maeneo ya kutupia, na moshi wa kuchoma taka vinaongeza hatari ya magonjwa, na kufanya maeneo ya karibu kuwa hatarini kwa kila mtu.

Angalau kwa upande wangu, sitaki tena kuishi karibu na maeneo hayo makubwa ya kutupa taka. Na pia nadhani kuwa masuala haya yanatuathiri sisi sote. Ninatoa wito kwa mamlaka kuchukua hatua dhidi ya tatizo hili.

2021 Location on Google Maps
1737958141138.png

2024
1737958165221.png

2018 Location on Google Maps
1737958206984.png

2024
1737958227465.png

2021 Location on Google Maps
1737958249257.png

2024
1737958552422.png
 
Kweli serikali ilifanyie kazi hili jambo. Kwa sababu maji hayo yanatumika sehemu mbali mbali na matumizi mbali mbali, hivyo wasipofanyia kazi athari kubwa has za kiafya zinaweza kutokea.
 
Map reading ... What are the possible economic activities taking place ?
1. Transportation
2. Agriculture
3. Fishing
4. Construction
5.

Tulozoea horizontal picture ni ngumu kuelewa aerial pictures
 
Nani anaeathirika na huo uchafu serikali au wananchi
Sisi sote! Hata serikali ni wananchi. Kwa hiyo hii ina maana kuwa hata barabara zikiharibika wananchi ndio wanaotakiwa kuzitengeneza kwa sababu wao ndio wanaotumia hizo barabara?
 
Serikali yapaswa kuingilia kati hili, maana wakazi wa Goba wenyewe sidhani kama watafanya. Wananchi ni kama wanafunzi ili jambo liende lazima walimu au wakuu wa shule waingilie kati. Viongozi wa Goba kuanzia nyanja za serikali za mitaa wajaribu kuhimiza utupwaji mzuri wa taka na watafute njia stahiki sio kutupa kwenye mto. Magonjwa ya mlipuko yakianza yatamlipua kila mtu hapo. Tahadhari ni bora kuliko tiba.
 
Uchafuzi wa mto Goba unaweza kuonekana kutoka angani. Hamuamini? Angalieni picha zilizo chini. Zinaonyesha picha za satelaiti za mto Goba. Kati ya 2018 – 2021, kulikuwa hakuna maeneo makubwa ya kutupa taka. Lakini ukilinganisha picha hizo na za mwaka 2024, utaona kwamba pembezoni mwa mto kunatumika kama maeneo makubwa ya kutupia taka.

Ni tishio moja kwa moja kwa afya ya umma. Maji machafu, taka hatari kutoka maeneo ya kutupia, na moshi wa kuchoma taka vinaongeza hatari ya magonjwa, na kufanya maeneo ya karibu kuwa hatarini kwa kila mtu.

Angalau kwa upande wangu, sitaki tena kuishi karibu na maeneo hayo makubwa ya kutupa taka. Na pia nadhani kuwa masuala haya yanatuathiri sisi sote. Ninatoa wito kwa mamlaka kuchukua hatua dhidi ya tatizo hili.

2021 Location on Google Maps
View attachment 3215299

2024
View attachment 3215300

2018 Location on Google Maps
View attachment 3215301

2024
View attachment 3215302

2021 Location on Google Maps
View attachment 3215303

2024
View attachment 3215310
Hapa ndio najiulza faida ya serekali za mitaa ni zipi!?
kama ubunifu wa kuboresha ,mazingira haupo
 
na hili nalo mnataka serikali ilisimamie? shit hole country serikali yenyewe iko bize kusiiana na kupakana mafuta kuwa wanaupiga mwingi ,yaani lana juu ya laana naanza kuamini maneno ya Trump, mwamba kabisa yule.
 
The greenery is diminishing very fast...is there anybody caring! Halafu tuna Wizara nzima ya mazingira. Too pathetic to know that kuna nguvukazi ya vijana wetu inafungiwa JKT wakati hizi ndio zilitakiwa kuwa KPI zao. Naungana kabisa kuwa hii ni SHITHOLE country!
 
Unajiuliza, hivi sisi tunaweza nini..hupati jibu.
 
Back
Top Bottom