Mtori ndio kwanza ndizi zipo kwenye fuso

Sakapara

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2019
Posts
299
Reaction score
397
Lazima Kujipongeza kwa kuweza kuanza Ligi kwa kucheza mechi za Ugenini mbili mfululizo kwenye viwanja vinavyotaka aina moja tu kucheza ambayo sio mchezo wa Simba kabisa, ndio maana utaona Wengine wanatoa lawama kwa Wachezaji au makocha ila huu ndio mwanzo wa Ligi na Tushukuru hatujaweza kupoteza mchezo hata mmoja ila tukubali pia hatujaweza kucheza vizuri maana hali halisi haitaki hivyo.

Tunarudi Nyumbani kucheza na Biashara 20/09 Jumapili halafu 26/09 Jumamosi na Gwambina ni muda wa kutuliza akili na kuweka neno NGUVU MOJA mbele tuwe pamoja hakika mnakwenda kuona Kandanda safi na ushindi mzuri zaidi huku wenzetu wengine nao wana kwenda Ugenini mechi mbili mfano Azam wanaenda Mbeya game zote Mbili wakati Yanga wanaenda Kagera halafu Morogoro dhidi ya Mtibwa haya yote ni ndani ya week hizi mbili na viwanja vitakuwa hivihivi tunapisha tu.

Tuwe wavumilivu kama kawaida yetu sio muda wa kejeli na misuguano sasa ni kuangalia mechi zijazo ndio muhimu haya yameshakwisha hii ndio FOOTBALL.
 
POINT 4 KWA MECHI 2 ZA UGENINI TUJIPONGEZE [emoji881][emoji1434]
 
Mnaijisifu vipi kwa matokeo haya wakati Game ya kwanza mlibebwa, refa alikataa goli la wazi kabisa.

Mkicheza pasipo kubebwa matokeo yenu mengi ni draw.
 
Mnaijisifu vipi kwa matokeo haya wakati Game ya kwanza mlibebwa, refa alikataa goli la wazi kabisa.

Mkicheza pasipo kubebwa matokeo yenu mengi ni draw.

MALALAMIKO FC tumewazowea toka lini wakaitakia mazuri Simba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…