Mtoto abakwa, maiti yatupwa kisimani

Mtoto abakwa, maiti yatupwa kisimani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
WATU wasiofahamika, wamembaka mwanafunzi wa darasa la tano na kutupa maiti yake katika kisima chama maji.

Kaimu Kamanda wa Polisi, mkoa wa Tabora, Anthony Ruta, amewaeleza waandishi wa habari kwamba mtoto huyo alikuwa amekwenda kuchota maji katika kisima hicho.

Kwa mujibu Kamanda Ruta,mwanafunzi huyo alibakwa na kuaga dunia Jumatatu saa 12 jioni katika kijiji cha Utakuja, Kata ya Itetemya katika Manispaa ya Tabora.

Ruta amesema, mwili wa mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miaka 17, ulikutwa na majeraha sehemu kadhaa. Amesema, hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo la mauaji.

Katika tukio lingine, mwanamke, mkazi wa Mangungu, wilayani Igunga, Lembe Lujiga ameuawa akiwa nyumbani kwake kwa madai ya imani za kishirikina.

Ruta amesema,watu wasiojulikana walimuua mwanamke huyo kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali, lakini kuna madai kuwa, chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina.

Ametoa mwito kwa wananchi watoe taarifa kuhusu mtu yeyote watakayemhisi kuhusika na mauaji hayo.

http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3951
 
Ish... Wa2 wakatili. My thoughts go to the family and relatives of the girl. But y r these ol happening? Y?
 
Binadamu siku hizi tumekua na roho za kinyama kuliko hata hao wanyama, watu wanafanya matendo ya ajabu bila hata ya kumuogopa mungui muumba. Hivi ina maana siku hizi binadamu hatuendi kumuabudu mungu au tatizo ni nini? tukisema tamaa si kweli maana wapo watu wazima wengi tu tena unamchukua kwa ridhaa yake, mbona sasa hivi hivi vitendo vya kikatili vimekithiri katika jamii zetu tofauti na zamani? Ee Mwenyezi Mungu wape watu wako moyo wa huruma na kukukumbuka wewe, binadamu tumekusahau ndio maana tunatenda yote haya. Pia nadhani watumishi wa mungu hawafanyi kazi yao sawa sawa, maana watu wamekua na roho za kinyama. hebu tumrudie mungu jamani haya yote yatakwisha. Tumesahu kuwa kuna moto tukifa
 
jamani kweli mtu unabaka mtoto mpaka unamuuua mmh adhabu tutakayokutana nayo huko ni balaa
 
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Na huyo aliyebaka mpaka kuua wala hatashikwa na akishikwa atakaa ndani siku 2 atoke jamani tunaelekea wapi nchi yetu hii na watu wake???
 
MHH!Kuna kitu hapa zaidi ya kubaka...! Haiji akilini kama watu katika hali ya kawaida wanaweza kufanya jambo la hivi...God 4bid!
 
HHHHHAAAAAAAAAAA!!! hii Minjemba wanawake wamejaa sana hata vitabu vya dini vimekataza!! Wakifika kwa Baba watakiona.
 
Back
Top Bottom