Mtoto ambaye hakunyonya maziwa ya mama

Mtoto ambaye hakunyonya maziwa ya mama

MAKALA

Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
47
Reaction score
12
Habari
naomba kujua ikitokea kua una mtoto ambaye hakunyonya kabisa maziwa ya mama, yaani ambaye anakulia kwa kutumia maziwa ya kopo, ni aina gani ya lishe? (chakula) inashauriwa kumpa ili kumuimarisha zaidi kiafya ukiacha hayo maziwa ya kopo anayotumia.

Mtoto umri wake ni miezi sita.
ahsante.
 
Habari
naomba kujua ikitokea kua una mtoto ambaye hakunyonya kabisa maziwa ya mama, yaani ambaye anakulia kwa kutumia maziwa ya kopo, ni aina gani ya lishe? (chakula) inashauriwa kumpa ili kumuimarisha zaidi kiafya ukiacha hayo maziwa ya kopo anayotumia.mtoto umri wake ni miezi sita.
ahsante.

Kwa umri wa miezi6 unaweza kumwanzishia uji wa lishe lakini kwa kuanza na mchanganyiko wa vitu vichache kadri anavyozoea unaongeza ingredients nyingine.

unaweza kupata unga uliotengenezwa tayari kwa watoto madukani au kuandaa vitu na kwenda kusaga mashine.

Vitu vinavyochanganywa kwenye unga wa lishe ni mahindi yasiyokobolewa, ulezi, karanga, ngano, mchele, soya na dagaa ukipenda ( wapo ambao hutumia uwele/mtama badala ya ulezi)

Hii ni kwa moni yangu tu ndugu waweza pata maoni tofauti, kila la kheri!
 
kwa kuanzia wiki2 za mwanzo mpe uji mwepesi sana na ulio iva sana wa sembe changanya na maziwa ya ngombe au yakopo
baadae mpe uji dona na maziwa.

kisha kila mwezi ongeza kimojawapo kama mchangiaji wa juu alivyo vitaja.
kumbuka kutengeneza uji mwepesi sana na uliopikwa mda mrefu kusaidia mmeng'enyo tumboni.

chuja unga kupata unga laini sana kabla ya kpika
 
kule kijijini mtoto wa miezi 6 wanakandamiza na ugali................... ukilicheki toto limenenepa utashangaa
 
Back
Top Bottom