Huo labda ni utaratibu wa hospital za serikali nchini tu!
Kwa hospitali za binafsi mara tu baada ya kujua hali hiyo wangemshauri wakitoe mara moja!
Sent using Jamii Forums mobile app
Poleni Sana mkuu Mkoa gani mkuuNdugu yangu wee, Ahsante sana na ndio sababu nikakimbilia kuja kupata ushauri
Lkn cha kuzingatia ni kuwa Hospital tulioenda ndio hospital kubwa hapa.
Sent using Jamii Forums mobile app
AminaPoleni Sana.
Inaonekana sheria zinatofautiana, maana kama nchi nyingine wanaweka maslahi ya mzazi/mama mbele zaidi.
Nikuvumilia tu, ila anahitaji uangalifu wa karibu kutoka kwa mume na ndugu....
Asije kukutana na wasiojua wakamuuliza....eehh naona tumbo linazidi kukua, hongera lini unatuletea mtoto?
Hii kauli inaumiza na anaweza kukosa jibu lakumpa mtu inategemea mko na ukaribu upi.
Mungu amtangulie amalize hiyo safari salama na ampe nguvu na afya ya kujaribu tena kubeba ujauzito.
Kimsingi kiumbe tumboni huwa hakiozi haraka na hizo 14 inawezekana ila kama itashindikana itabid wamuongeze uxhumgu kwa njia ya dawa ila pia wanaweza mfanyia c section yote kunusuru hari ya mama
Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikuwaje mkuu?Umenifanya nikumbuke maumivu ya kumpoteza dada yangu sababu ya mtoto kufia tumboni
Mkuu Fanya hima nenda Hosp zinazoeleweka vinginevyo yasije wakuta yaliyotukuta
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ungekuwa mama ungejisikiaje kubebelea kiumbe mfu kwa wiki mbili?Watu humu wanaona ushauri huu kwa hisia umetoka hospitali ya serikali kwa nadharia ya kwamba hawajali.
Ila kuna vitu vingi vinafanyika hospitali za binafsi si kwa maslahi ya mgonjwa bali kwa maslahi ya hospitali.
Na kwa sababu wengi tunaaminishwa hivyo tunaamini huko ndiko salama, si kweli.
Hilo jambo la kawaida kusubiri.
Kwa sababu akianzishiwa uchungu ikaleta shida inabidi azalishwe kwa operation kitu ambacho ni shida kubwa katika sura zote.
Ukianza wenyewe chance za kujifungua bila shida ni kubwa zaidi ingawaje vyote vinawezekana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Habari za Mda huu wakuu wote humu ndani,
Ni matarajio yangu weekend inaenda swadacta na mapumziko yapo sawa sawia
Naomba msaada juu ya swala lililo mtokea Shemeji yangu (Mke wa kaka yangu),
Shemeji yangu huyu yeye ni mjamzito na ujauzito wake ulifikia miezi saba,alihisi mtoto apigi tena tumboni na akawa anahisi maumivu ya kichomi tumboni na hata akifanya shughuli za kuinama ( kama kufagia,kuosha vyombo n.k) alikua anahisi maumivu makali sana, Hivyo akapata wasiwas na kuamua kwenda hospitali kwa ajiri ya kufanya Ultra sound,
Bahati baya zaidi majibu yakatoka kuwa mtoto amefariki, kwasababu alienda ktk zahanati tuu, akashauriwa aende cliniki aliyokuwa ameanza kwenda ili akapewe rufaa ya kwenda hospital kubwa kwaajiri ya kwenda kuzalishwa na mambo kama hayo,
Kweli alipewa rufaa na kwenda huko hospital kubwa, baada ya kufika huko waliziona zile documents zote na kuthibitisha hilo, lakini sasa waka mwambia, madhari mtoto amefariki tumboni, hivyo uchungu huwa unakuja wenyewe automatic,
Hivyo wamempa siku 14 na kumwambia endapo zikamaliza hizo siku kumi na nne kama hajapata uchungu aende wakamzalishe, leo ni siku ya tano hana dalili zozote za uchungu, sasa nilikuwa naomba msaada kwa nyinyi wataalamu,
Je hii ya Mama mjamzito kukaa na kiumbe kilichokufa tumboni zaidi ya wiki sasa haitaleta madhara ya kiafya kwake baadae!? kama vile kuoza kwa mtoto na baadae kuoza kwa kizazi n.k
Lkn pia Je ni kweli lazima apewe hizi siku kumi na nne kwanza? ili apate uchungu mwenyewe!?
Mwisho kabisa Je kunauwezekano wa njia nyingine kutumia zaidi ya kusubiri hizi siku 14!?
Natanguliza shukrani za dhati.
Ahsante.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kupewa option ni jambo muhimu. Mara nyingi nafasi ipo. Lakini si mara zote huleta matokeo chanya.Wewe ungekuwa mama ungejisikiaje kubebelea kiumbe mfu kwa wiki mbili?
Binafsi nisingeweza
Hospital wangempa options zikiambatana na sababu za kila option
Mama atachagua mwenyewe!
Kwa hiyo hospital ikishakuwa ni ya serikali basi daktari ndiye msemaji wa mwisho