Mtoto ameover dose antibiotic

Loeli

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
997
Reaction score
763
Wakuu toeni msaada wa haraka. Mtoto wa miaka 8 aliandikiwa amoxyline (spelling) capsule moja kila masaa 8. mzazi wake amempa saa 8 leo na ilikuwa apewe tena saa nne usiku. Kwa bahati mbaya wakati anampa dawa saa 12 jioni akawa amempa tena amoxyline badala ya saa nne usiku. Mzazi amepanic sana. Naombeeni msaada je apewe maziwa kupunguza makali ya dawa au kuna first aid nyingine? mtoto amechangamka tu. Tafadhali saidia. MziziMkavu njoo huku please.

Update at 00:03
Wakuu mtoto hali imebadilils. Baada ya kupewa maziwa jasho lilimtoka. Akakaa kidogo shingo ikaanza kwenda upande. Baadaye ikawa inatizama juu. Wazazi wamempeleka hindu mandal na dr amesema hakuna tatizo la overdose. Ameandikiwa referal aende amana ili aweze kwenda muhimbili kwa ajili ya shingo kukakamaa kwa muda wa say dk 10 na kurudi kawaida. Wamemrudisha mtoto nyumbani ndiyo tuko hapa kupiga hesabu. Hindu mandal dr aliwaambia pia kama wanawezs pata wataalam wa kienyeji!!!! huku wakienda muhimbili kwa CT scan. Please wenye uzoefu saidieni hili la kukakamaa shingo ni kitu gani!
 
Wakuu njooni jamani. Huyu mama analia na kuogopa sana. Ndiyo ameshachemsha maziwa ya ng'ombe mtoto anakunywa. Nimemshauri ampe pia maji mengi sana akojoe.
 
Haina shida hata kidogo wala hana haja ya kumpa maziwa. Mi mwanangu wa miaka 2 aliwahi kubugia kile kichupa cha Amoxiline ya syrup chote kikiwa kimejaa na wala hakikumdhuru
 
Tulizana,na jaribu kumpa mama na kijana maneno ya faraja atulie kwa kuwa masaa karibu matano yamepita, ile dozi ya kwanza imeishapungua kiasi fulani, ila asirudie kumpa dozi nyingine saa nne usiku,usimpe maziwa kwa kuwa dawa haiko tumboni kwa sasa mpe maji kwa wingi.msiwe na wasi wasi hakuna hatari ki hivyo!.Pamoja sana.
 
awe na amani.katika hiyo dawa...therapeutic range yake (mpaka wa kusababisha madhara makubwa ya sumu) ni.mkubwa mno hivyo asinywe maziwa ataoharibu dawa bure.
 
mpatie maji mengi awe anakunywa taaratibu ili aweze kukojoa sana.
 
Wakuu sasa mtoto ame develop tatizo la shingo kukskamas on and off. Hindu Mandal wamesema haihusiani na overdose. Wameshauriwa waende muhimbili. Tuko hapa mtoto sasa amelala. Je inaweza kuwa tatizo gani. Hana homa na malaria alipima temeke hosp na hindu mandal hana. Ila kuna watu wamesema rapid test ya malaria wakati mwingine inakosea hivyo wameshauri wazazi watumie maambara zenye kutumia microscope.
 
Wakuu mkiamka wenye uzoefu wa kujua causes ya shingo kukakamaa on and off watusaidie. Hili tatizo halijawahi kumtokea toka azaliwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…