Mtoto Anatoka Wapi?


Pundit,
You are right.. watoto wa siku hizi are not dumb or stupid.Ukimdanganya na huku yeye anajua au ataambiwa kwingine.. will never trust you again!
Big mistake parents.
 
Tunafundishwa kuwa tusiwaambie uongo watoto ni vyema ukapima kila neno unalomwambia mtoto wako mdogo kwani hicho ndio kipindi chake cha kusoma na kujifunza. Ingawa ni watoto lakini inafika mahala wanajua kuwa Mama ama baba anadanganya na hapo hatakuwa na hamu tena ya kuuliza. kitendo chako hicho kianweza kumpunguzia uwezo wake wa kufikiri, kudadisi na kepembua mambo. Malezi mazuri ya watoto yanaanzia katoka umri kama huu. Ni vyema tukawa waangalifu katika majibu yetu, ingawa si kila suala linahitaji jibu sahihi lakini ni vyema tuelewe tunakowapeleka watoto wetu .
 
Matusi kuwatukana sawa, lakini "matusi" ya kuwafundisha baiolojia mwiko!
...Pundit vipi na wewe??? Kumtukana matusi mtoto ni sawa? Big NO!!! unamfundisha au unatengeneza kitu hapo?? bailojia ipi kumwambia mtoto kuwa mtoto anapatikana kwa mungu?? Lipi lenye afadhali kusema mtoto amenunuliwa baharini au alitoka kwa mungu???? Msitengeneze kizazi danganyifu angalau ufundishe vyenye muelekeo wa ukweli kidogo katika imani.
 
Very true!
My son once asked me. 'Mum, there are two types of giving birth, one is ceasarian section and the other one is ....sema wewe mama, he didn't want to say it ffrom his mouth! I asked how did you know? Kumbe DSTV wanaonyesha eac and everything!!!
And after sometime he told me, 'mum, when you lie to me, i see it on your face'!!!!
Kids know more than what we think! For sure this is very true!
 

Kipanga usiwe kama kilaza asiyeweza kusoma haiku,

Matusi kuwatukana sawa, lakini "matusi" ya kuwafundisha baiolojia mwiko!

Kuna mtu alieleza jinsi alivyosikia mama anamtukana mtoto matusi, mimi ndiyo nikasema hapo juu kwamba it seems kuwa tuko OK kuwatukana watoto matusi lakini hatuko OK ku explain birth kwa misingi ya kuwa ni "matusi"

Kama unajua kusoma, hebu soma post yangu ya juu kuhusu kuwaambia ukweli watoto. Inaelekea wewe si msomaji sana humu, kwani kama ungekuwa msomaji mzuri ungeshajua kuwa siyo tu mimi sikubali uongo wote unaohusishwa na mungu, bali pia siamini kuwako kwa mungu period.

Sijui hayo unayoyasema na kunipachika mimi umeyaokota wapi, au kuna mtu mwingine anapost kwa jina la Pundit humu?

Vipanga kawaida wanajua kusoma na comprehension, wewe kipanga wa wapi?
 

Bubu Pointi yako nzuri lakini ilifanya kazi kipindi kile cha ujamaa..Sasa wakati huu wa utandawazi ni vigumu.
Na watoto kama kawaida wa kizazi hiki wana maswali BALAA!
 



Duh! unafananisha hata ambavyo havistahili kufananishwa!!! 😕
Wacha wabongo walalamike kwamba neno fisadi linatumika hata pale ambapo halistahili kutumika!!!!

Mafisadi waliokupua mabilioni ya pesa na kutomwambia mtoto wa chini ya umri wa miaka 10 mtoto anapatikanaje mbona havishabihiani hata kidogo!!! Kutomwambia mtoto wa chini ya umri wa miaka 10 jinsi mtoto anavyopatikana ni kuinsult his/her intelligent!!!! Hmm!!! labda mimi ni wa mwaka 47!!! Mtoto wa chini ya umri wa miaka 10 ukamwambie jinsi mtoto anavyopatikana ili iweje hasa? Ndiyo awe na akili nyingi sana!!!!!!? Mwe!!!! Kwa hiyo wale ambao hawakuambiwa kuhusu hiyo process ni mabumbumbu wa kutupa!!!!

Siye ambao wazazi wetu hawakutwambia process ya jinsi mtoto anavyopatikana tulipokuja kujua proceess hiyo hatukuwaona wazazi wetu kama ni waongo wala mafisadi!!! Na watoto wetu pia walipofikia umri wa kufahamu hayo hawakutuona waongo wala mafisadi!!! Na wanawake wala hawakuwa malaya wengi wao wamekuwa watu wenye umuhimu mkubwa katika nchi yetu, pamoja na kuwa hawakuambiwa process ya jinsi mtoto anavyopatikana walipokuwa na umri mdogo.

Ndiyo maana mimba za teenagers zimeongezeka kwa kasi kubwa duniani kote kwa sababu ya watoto wadogo wanaambiwa process ya kupata watoto mapema kuliko inavyostahili. Unakakuta kabinti kana 12 na kenyewe kanasema kanataka mtoto!!!!! "Yes, I want my own baby and I can take care of her." Unabaki mdomo wazi.

Sijui syllabus za shule zetu siku hizi, lakini process ya kupata mtoto ilikuwa haifundishwi mpaka secondary. Sasa leo wazazi wanataka wamwambie mtoto wao ambaye hajatimiza hata miaka 10 process ya kupata mtoto!!! kisa watoto wa siku hizi wako smart sana watajua tu!!! lahaula!!!! Kwa wale mlio majuu mambo haya yanafundishwa madarasa ya chini mno na labda hili la kufundisha mapema limechangia mno ongezeko la mimba za watoto. Halafu unasikia wazazi wanalalamika watoto wa siku wanayaanza mambo mapema mno!!! Sisi hatukuwa hivyo!!! Kumbe wakulaumiwa ni wazazi wenyewe kwa kuwaambia watoto wao mambo wasiyostahili kuyajua katika umri mdogo, kusoma magazeti au vitabu vilivyozidi umri wao na kuangalia vipindi vya TV ambavyo hawastahili kuviangalia.

Mushi, swala hili halihusiani na ujamaa wala ubepari bali ni maadili mema ya utamaduni wetu ambao hauna kasoro yoyote kuhusiana na kutomwambia mtoto wa umri mdogo jinsi mtoto anavyopatikana.

Mkumbuke, wazazi wana viwango tofauti katika kulea watoto wao. Wakati wengine hawaoni umuhimu wowote wa kuwaambia process mtoto wa chini ya miaka 10 au hata zaidi, nyie mnaona umuhimu wa kufanya hivyo kwa kuogopa kuonekana waongo na mafisadi kwa watoto wenu endeleeni kufanya hivyo.
 
Come on Mizozo this is to a kid ... then you will have a lot of explaining to do i.e. show the kid the shamba what do you do shrink ???????????

Dah Naima,

Nilikuwa katika long vacation na leo jmosi ndo mekuja huku Visiwani kuimaliza utamu... Sasa ngoja nimalize kusoma mjadala mzima kisha nitakuja na kukufafanulia husiana na shamba la watoto cna kila kitu...

Am I?...Shrink.
 
Suala zima hapa ni kwa watoto kutaka kusaidiana kupata ufahamu husiana na suala zima la mtoto anatokea wapi?

Kama ambavyo nimesoma michango mingi, nami naungana na wote wanaosema kwamba mtoto anadeserve kuambiwa ukweli...wa kila kitu. Lakini jinsi ya kumwambia mtoto ukweli halisi wa mambo inatakiwa utofautiane na jinsi cambavyo utampa ukweli a grown ups. Na swali la kwamba mtoto anatoka wapi sio swali ambalo utatakiwa kumjibu mtoto mara moja na ukawa umemaliza. Tunatakiwa kujaribu kulijibu hili suala zima sambamba na ukuaji wa mtoto.

Kutokana na sisi kuwa tunashindwa kufikisha ukweli muafaka kwa wakati muafaka kwa walengwa ndio maana katika jamii yetu hata Elimu juu ya Ukimwi inakuwa ni shida sana kueleweka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…