mtoto halali usiku

millionroses

Member
Joined
Nov 12, 2012
Posts
19
Reaction score
2
habari wana jf....nimejaliwa kupata mtoto wa kiume ambaye kwa umri ana mwezi na nusu sasa...mchana kutwa anashinda amelala akiamka ni kunyonya na kuendelea kulala..amekuwa akilala hadi saa tano au sita usiku baada ya hapo akiamka ni halali tena ikibidi hadi asubuhi...kwakweli napata shida sana....Naomba msaada wenu..je hii ni kawaida kwa watoto wote au wangu ana tatizo????
 
Kawaida but jatibu kumbadilishia ratiba za kulala.
 
mkuu skidemount unamaanisha niwe namuasha wakati mwingine anapokuwa amelala????
 
Jibu hapa ni ndiyo kwamba usimuache alale mchana kutwa tafuta namna ya mtoto kulala masaa labda matano mpaka saba mchana ili aongeze masaa ya kulala usiku. Pia kuna uwezekano labda hashibi usiku na hali hiyo inasababisha ashindwe kulala.

mkuu skidemount unamaanisha niwe namuasha wakati mwingine anapokuwa amelala????
 
pole. mtibulie ratiba yake kidogo ya kulala ili alale na usiku...
 

Kwa kulala mchana bila kulialia inamaanisha hana tatizo, angekuwa anaumwa hata mchana angelia

1. Njaa huwasumbuwa sana watoto hasa masaa ya usiku na maranyingi akinamama huwa wamechoka kunyonyesha mchana, nawakihitaji kujipumzisha. Jaribu kutafuta source mbadala ya lishe kwa muda anaolia (mfano maziwa ya aspen yanapatikana kulingana na umri wa mtoto) akipewa akashiba kama shida ni njaa atalala mazima mpaka asbh. Note/zingatia usafi ni muhim sana.

2. Kama No-1 juu itashindikana, chunguza malazi yake hasa vilalio, mkojo nk, watoto hawapendi kabisa mkojo au vitu vinavowasha na kuchoma maka mkojo, hakikisha kila anapojikojolea maramoja anabadilishiwa viwalo, kama hili ni tatizo atalala

3. Kama No-1 & 2 itashindikana, jaribu kuangalia mazingira yanayomfanya alale machana, upatikanaji wa hewa safi, mbanano nk, hata hivyo mara zote mtoto afunikwe vema hatakama kuna joto kuzuia baridi kumpatia vichomi mtoto yaan pneumonia ambayo huwapata watoto wengi kwa kuachwa wazi na wazazi wao wakzani wanawapungisha upepo kumbe nikosa kubwa.

4. kama anakaumri kakubwa kidogo jaribu kumdistable/kumsumbuwa masaa ya machana asilale saanaaaa alale usiku japokuwa hii sio mbinu sahahi mtoto anatakiwa apate usingizi mnono kwa ukuwaji bora.

tatizo likiendelea waone mabibi tofauti tofauti kama watatu au wanne kwa ushauli zaidi


Asalamallekum mdau.
 
Kwa umri wake ni sawa huwa vinalala sana mchana lakini usiku lazima mkeshe we jaribu kumchunguza anapolia usiku ukimpakata hawezi kulia anataka tu awepo mikononi na akuone ukimlaza tu kosa,
Source: sisi wazazi sugu.
 

Nakubaliana na hii hoja. Mwanangu ana almost mwezi na silali usiku. Usiku wa leo sijalala tokea saa tatu hadi kumi na moja alfajiri. Mama yangu akaamua kumnyesha mtoto maziwa ya sma ndo tukalala baada ya kumbembeleza kilio chake cha hatari. Ila saa nyingine mtoto anashindwa ku switch btn nipple ya mama na nipple ya chupa kwa hiyo kama wangu ukimpa chupa anashindwa kuvuta/ku suck. Mama alimywesha na kijiko ilipotokea hali hii. Pole sana
 
asanteni kwa ushauri lakin sasa kama mjuavyo kila mtu huwa na wazo lake kutokana na ulezi wake kwa watoto wa kiume...baadhi ya watu wangu wa karibu wanasema ana CHANGO ndio linasababisha asilale usiku kwani huwa kama anajikunja kunja na kama ana gugumia hivi....binafsi nilimpeleka hospital nikaambiwa ni gesi ndio inakuwa inasumbua na sio jambo la kutisha kwani nilielekezwa cha kufanya na pia nikapata dawa ya kutuliza....Sasa kuhusu hilo CHANGO ndio sielewi sasa?? nabaki kuchanganyikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…