SHOSHOLOZA
Member
- Jun 28, 2012
- 39
- 2
Ndugu zangu naomba msaada wa kisheria nina mtoto wangu kabadilishwa jina na kupewa la baba wa kufikia, nikiongea na mama yake anasema kwakuwa silipi ada ya mtoto (12yrs) na huyo bwana analipa ndo maana ikawa hivyo.
Naomba msaada wa kisheria uu ya hilinianzie wapi, ilinisaidiwe.
Asanteni
Naomba msaada wa kisheria uu ya hilinianzie wapi, ilinisaidiwe.
Asanteni
Pole sana.
Kwa uelewa wangu ni kwamba, hapaswi au haruhusiwi kisheria kubadili jina la mzazi mwenzie lililoandikwa kwenye hati ya kuzaliwa(birth certificate) bila idhini ya mzazi mwenzake isipokuwa kwa sababu fulani(exceptions).
Kama nilivyokuelewa kwenye maelezo yako kuwa mama ndiye mwenye sole custody na ana-discharge sole parental rights and responsibilities (wakati wewe upo na hutekelezi majukumu hayo kwa mtoto), na kuwa kuna mtu mwingine anayatekeleza majukumu hayo kwa muda mrefu bila kuingiliwa na mtu yeyote(wewe)...mama anaweza kubadili jina la mtoto ikiwa ni kurahisisha huduma muhimu kwa mtoto kama kupata hati za kusafiria,ada n.k kwa kuapa na kusaini statutory declaration kwamba yeye ndiye sole legal parent na ndiye anaprovide legal custody bila wewe.
Lakini kama ingekuwa wewe unatoa huduma kama itakiwavyo basi angepaswa kupata ridhaa yako kabla ya kufanya hivyo.
Nakushauri,thibitisha kwanza kama kweli ni mwanano, pia hata kama umeachana na mkeo, timiza majukumu yako kwa mwanao na mkeo wa zamani kwa kumlea mtoto...hapo atapaswa kukushirikisha jambo lolote lenye kuathiri mambo yamuhusuyo mtoto.
Sababu nyingine za kubadili jina zaweza kuwa ni kuwa mwenzi wako anaweza kusaini hati ya kubadili jina la mtoto kwasababu labda una tabia mbaya,mgomvi kwake,hujali familia(umeitelekeza) au kuendelea kutumia jina lako itaathiri makuzi ya mtoto n.k
Kifupi, timiza majukumu yako.