Mtoto kugoma kucheza tumboni

Asante doctor yaan hapa sijielewi kabsa ngoja kesho nimuwahishe hospital
Yaani kesho mbali sana. Hiyo siyo dalili nzuri. Mtoto anapata kitu kinachoitwa fetal distress. Ikitokea hali hiyo madaktari wanakazana kumwokoa mtoto kwa maji ya uchungu au hata Ceasarian Section (Upasuaji). Nayajua, sikutanii, yalishatukuta. Kesho mbali sana mtoto asipocheza anaanza kukosa oxygen tumboni. Sitaki kukutisha ila naomba nikushauri kwa kuwa nayajua!
 
Wakati mwingine hata madaktari wanafanya vitu vinatupa mashaka.Shemegi yenu kama wiki 2 au wiki na nusu imepita aliamka akasikia kama maji yanatoka akahisi ni damu lakini alivyotizama ni maji,Ni mja mzito miezi 9 na makadirio ni tareha 8/7/2019.Nipo mbali nikamshauri aende hospitali akaenda sinza palestina wakamuweka muda mrefu sana nikajua atalazwa usiku kama saa moja wakamtoa.Walimuambia ana U.T.l.wakampa dawa anatumia lakini ile hali ikasita kidogo.

Jana akaamka na hali hiyo tena nikamsishi aende hospitali akaenda pale pale sinza,wakamuambia arudi nyumbani akiona maji mengi arudi hospitali.Hali ile ikaendelea mchana wote ila ni kidogo kidogo sana ikabidi nimpigie DR wake Karatu akasema sio dalili nzuri nimuwahishe hospitali.Jioni akaenda tena pale pale wakamuweka wodini bila ruhusa ya simu.Alienda na mama mkwe ila alijiiba kubaki na simu.Usiku saa 7 wakampeleka mloganzila.

Tangu usiku huo hadi muda huu hawajamfanyia chochote.Waliandika dawa anunuliwe ya uchungu,phamarcy kwao hawana,watu wakahangaika kuna Pharmacy nyingine jirani wakakuta pamefungwa leo jumapili.Nikahangaika Fabrek,Faru sijui Falu manzese hawana ikapatikana sinza.Kama wamemuweka masaa yote hayo bila huduma yoyote kuna tofauti gani kubaki nyumbani hadi jioni hii?uzuri anasema mtoto anacheza.Madaktari ni nini hiki mimi sielewi na nipo mbali sijalala usiku na sina hata hamu ya kula leo.
 
Pole mkuu pole sana..! Lakini je mtoto na mama wanaendeleaje? HOPE AMEJIFUNGUA SASA
 
Pole mkuu pole sana..! Lakini je mtoto na mama wanaendeleaje? HOPE AMEJIFUNGUA SASA
Leo saa nane usiku tumepata mgeni wa kike,Wanaendelea vizuri ila hawajaruhusiwa.Tulinunua dawa za uchungu akapewa usiku tukajaaliwa.Mgeni wamempachika jina manesi na wazazi wenzie wanamuita chibonge kabla hata mimi mwenyewe sijatoa jina.Wamesema hawataruhusu mama na mtoto kutoka wanamuangalia chibonge maana inawezekana alikunywa maji machafu baada ya chupa kupasuka kidogokidogo,Watakaa siku mbili pale kwa hiyo wapo mloganzila wodi namba nne ya wazazi.Karibuni sana.
 
Tumshukuru Mungu mkuu. Nimefurahi sana
 
Mkuu wahini sasa hivi Hospitali,asee mimi wife ilimkumba hali hiyo hiyo tena miezi tisa kabisa, tukapoteza jembe..maana mtoto alitoka hana uhai tena..ni kitu cha miezi miwili imepita,imeniuma sana siwezi kueleza.
Pole sana
 
Mpaka imefika miezi 9 ni lazima atakuwa anajua mtoto anacheza akila chakula gani, akisikia sauti gani au mziki gani.

Kama hakuna reaction kwa vitu hivyo, wahi hospitali muone gynaecologist.
Kumbe..mtoto huwa anasikia sauti akiwa tumboni?
 
Hongera baba chibonge
 
Uzazi wa kwanza usikie tu mwenzako, pole sana mkuu na hongera pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…