mtoto kugoma kula

mamD

Member
Joined
Apr 9, 2014
Posts
9
Reaction score
3
habari zenu wadau, nina mtoto wa mwaka mmoja na miezi saba lakini ni mbishi wa kula chochote, ana ratiba ya milo sita kwa siku lakini sijawahi kumuona akila kwa raha ni kilio tu nifanyeje? Uzito wake hauridhishi ana 11kgs sasa hivi. Natanguliza shukran kwa msaada!
 
Hiyo ni hatar maana anaweza pata utapia mlo huyo mtoto kama akiendelea hivyo.Mbadilishie aina tofauti tofauti ya chakula labda amechoka hicho chakula anachokula! Juisi yenye mchanganyiko wa palachichi itmsaidia pia kuongeza aina tofauti tofauti ya vitamins. Pata ushaur wa daktar kama anaweza kula dawa ya kuongeza ham ya kula. Kampime pia minyoo!
 
Uwe unafanya kama unamsifia kuwa kwamba yeye ni mtoto mzuri tena unamwambia kuwa watoto wazuri ndio wanaokula na sifa zingine ili mradi tu ale, pia jaribu kuangalia aina ya chakula alacho huenda kikawa kinamchosha jaribu kumbadilishia vyakula mbalimbali vilivyopikwa vizuri.
Mara nyingi watoto kama hao wanaosumbua kwenye kula huwa na akili ndogo(Low IQ).Halafu unaposema mtoto ana milo sita kwa siku kwanini unafanya hivyo?
 
Uwe unafanya kama unamsifia kwamba yeye ni mtoto mzuri tena unamwambia kuwa watoto wazuri ndio wanaokula na sifa zingine ili mradi tu ale, pia jaribu kuangalia aina ya chakula alacho huenda kikawa kinamchosha jaribu kumbadilishia vyakula mbalimbali vilivyopikwa vizuri.
Mara nyingi watoto kama hao wanaosumbua kwenye kula huwa na akili ndogo(Low IQ).Halafu unaposema mtoto ana milo sita kwa siku kwanini unafanya hivyo?
 
milo sita ina maana kuwa saa 12asubuhi maziwa fresh, saa 2 chakula, saa 5 maziwa fresh, saa 8mchana chakula, saa 10 uji, anakaa free akinywa juice au tunda mpaka saa 2usiku chakula.
 
milo sita ina maana kuwa saa 12asubuhi maziwa fresh, saa 2 chakula, saa 5 maziwa fresh, saa 8mchana chakula, saa 10 uji, anakaa free akinywa juice au tunda mpaka saa 2usiku chakula.

Hapo nimekuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…