Mtoto Kulia bila sababu

Mtoto Kulia bila sababu

Indoraptor

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2019
Posts
249
Reaction score
506
Habari wakuu

Nina mpenzi wangu ambaye amejifungua miezi mitatu iliyopita lakini tangu ajifungue kumekuwa na tatizo la mtoto kulia kila saa bila sababu.

Nilimshauri aende hospital lakini hospital wamesema haumwi chochote, kama ni kunyonya ananyonya vizuri tu lakini tatizo hili limekuwa sugu sasa, yaani sio usiku sio mchana ni kulia tu kila mara.

Naomba msaada wa tatizo hili kwa wajuzi
 
Katika mila za kiafrika mtoto ni mali ya ukoo wa baba ikiwa na maana kuna mwunganiko wa kiroho na mababu na mabibi katika familia ya Mme. Hivyo kama mmekutana na mpenzi wako mpaka mtoto akazaliwa huna budi wewe baba umpeleke kwenu na akifika tu atanyamaza au utaambiwa cha kufanya ili anyamaze. Laa sivyo kama wewe ni mlokole au huna imani za kilokole basi akili kichwani kutokana na imani yako
 
Kulia kwa mtoto mchanga ni jambo la kawaida, wala siyo homa. Hali hiyo hutokea kwa miezi michache baada ya kuzaliwa, Hali hiyo wengine hupungua kuanzia miezi sita japo wengine wanawahi kuacha kuanzia miezi miwili tu
 
Shukran mkuu kwa ushauri wako huenda ikawa suluhisho
 
Kulia kwa mtoto mchanga ni jambo la kawaida, wala siyo homa. Hali hiyo hutokea kwa miezi michache baada ya kuzaliwa, Hali hiyo wengine hupungua kuanzia miezi sita japo wengine wanawahi kuacha kuanzia miezi miwili tu
Ni kweli, ila imekuwa too much. je, hamna tiba ya tatizo hili?
 
Mtoto analia Mara kwa Mara na bila sababu kwa jinsi uonavyo wewe, lakini ukweli no kwamba mtoto analia 1. Kuzoesha mapafu kufanya kazi Maana yalikaa miezi kadhaa (tumboni) bila kufanya kazi.
2. Anahakikisha baba hagegedi (hatmbi) hii husaidia kuepusha mimba na kuharibiwa kwa maziwa mapema.
 
Back
Top Bottom