gileun
Member
- Nov 8, 2017
- 85
- 74
Habari wakuu!
Nina mtoto wangu wa kiume kwa sasa yuko na umri wa mwezi mmoja na wiki moja. Dogo huwa analia sana wakati wa usiku hasa kuanzia mida ya saa nne usiku hivi. Siku kadhaa ilikua kulia kwake ni afadhali lakini jana ikawa ni zaidi ya siku zote,yaani kalia tangu saa nne mpaka saa nane kasoro usiku. Tungeweza sema anamaumivu ya tumbo lakini hapana maana hajikunji kunji wakati analia na zaidi ni kwamba kwa jana tulimnywesha na Sheladol kwa ajili ya maumivu maana tulihisi pengine kuna mahali panamuuma na hatuezi jua maana hawezi kutuambia. Swala la njaa tuliweka pembeni sababu alikua hata maziwa hataki kunyonya kabisa. Leo tumeenda kwa daktari kamcheki lakini dogo yuko sawa, daktari akashauri yawezekana huwa anapata mshtuko na pia wakati mwingine huwa sababu ana kiu ya maji.
Nashea uzi huu ili kujaribu kupata mwanga toka kwenu wataalam na wadau wengine juu ya nini tunaweza kufanya ili kwa kiasi kikubwa kuondokana na hili tatizo.
Natanguliza shukurani zangu za dhati kwenu!
Sent using Jamii Forums mobile app