Mtoto kuota MENO Vs Kuharisha

Mbeky

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2013
Posts
672
Reaction score
518
Wadau nimekua nikisikia kwamba eti mtoto akianza kuota meno huwa anaharisha.
Mwanangu mi alipoota vijino vinne vya mbele sikuona hiyo hali ila sasa ameanza kuongeze mengine naona choo chake kimeongezeka kuwa laini na sometimes ni kuharisha kabisa kila akijisaidia...tumempekela hospital wamempima choo hakina shida..malaria hana ila daktari akasema inaweza kuwa meno kuota...kwa kuwa alienda mama ake aliponipa suggestions hizo za daktari mi sijamuelewa kabisa.
Sa wadau kwa wenye ufahamu au experience na hali hii naombeni msaada wa mawazo.
Ni kweli kuota meno kunaweza changia mtoto kuwa na choo chepesi /kuharisha
Is it scientifically applicable au ni imani za mtaani tu
 
Meno yanapoota huwa yanawasha hv hivyo mtoto hupeleka vidole kujaribu kujikuna hivyo ni rahisi sana kupeleka na vijidudu vya magonjwa ktk mfumo wa chakula hivyo kupelekea kuharisha! Ikumbukwe pia mtoto hutambaa kwa kutumia mikono na kama sehemu si safi hupeleka uchafu mbalimbali kinywani.
 
Jibu la Dr Bulugu huenda likawa kweli, japokuwa watoto muda wote, hata kabla ya kuanza kuota meno huwa kila wakionacho au kukishika lazima kielekee mdomoni.
Kwa mtoto yeyote, shortest route ya mkono ile ya hand-to-mouth.
 
Ingawa watu wengi huamini kuwa mtoto akiota meno lazima ataharisha, hivi vitu havina uhusiano kisayansi...

Soma zaidi HAPA
 
Faeces are sometimes so liquid they are mistaken for urine. NB: it is normal for breastfed babies to have liquid stools. Some cow's milk causes harmless green stools. Diarrhoea may be an early sign of any septic illness.
 
Siku nyingine uwe unaenda na mkeo hospitali ili upate majibu directly from doctor.

Ni kweli mkuu...huwa najitahidi napopata nafasi tunaenda pamoja ila wakati mwingine majukumu yananibana...
 
Faeces are sometimes so liquid they are mistaken for urine. NB: it is normal for breastfed babies to have liquid stools. Some cow's milk causes harmless green stools. Diarrhoea may be an early sign of any septic illness.

Dr Bulugu huyu amesha quit breastfeeding anamwaka na miezi mi nne na nusu..
 

Basi kwa maelezo hayo ya vipimo basi huenda ikawa ni loose stool tu kwani pia kama ni kuharisha lazima utaangalia ni mara ngapi kwa siku, kwa siku ngapi? Nature ya stool, Kama kuna blood in stool, au kama ana dalili za upungufu wa maji mwilini km yupo irritable, macho kuzama ndani kidogo,ukivuta ngozi kidogo hasa ya tumbo kuchelewa kurudi, nk . Na km alitumia antibiotics hv karibuni huenda ikasababisha . Ila nataka kuamini hayo yote daktari alizingatia kumuuliza mama ndio maana kawahakikishia hakuna shida. Ila kpndi hiki mtoto aongezewe fluid intake kila aharishapo. Ahsante
 

Nashukuru mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…