Ziroseventytwo
JF-Expert Member
- Mar 27, 2011
- 8,581
- 15,618
Leo, Muda huu naandika huu uzi, kuna dada huwa anatuuzia chai kila ahsubuhi. Kaja ofisini kwake, lakini anadai anasikia homa kali, nilipomwambia aende kufanya vipimo akasema tatizo analijua. Eti mtoto wake aliyekuwa akinyonya kampigia chafya ziwa lake. Na akaendelea kusema ikiwa mtoto atapiga chafya au kucheua wakati akinyonya, hupelekea mama kupata homa kali na ziwa kuvimba. Hii nimewahi kuisikia kwa mama wengi wanaonyonyesha.
Sasa kitaalamu, hii dhana ipo? Na kama ipo kitaalamu inaitwaje? Kuna connection gani hapo inayopelekea mama kupata homa wakati mtoto ni wake na maziwa ni yake?
Sasa kitaalamu, hii dhana ipo? Na kama ipo kitaalamu inaitwaje? Kuna connection gani hapo inayopelekea mama kupata homa wakati mtoto ni wake na maziwa ni yake?