Mtoto kutolewa nje siku arobaini baada ya kuzaliwa.

Mtoto kutolewa nje siku arobaini baada ya kuzaliwa.

Mnyaluhala.

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
1,430
Reaction score
1,785
Habari wadau. Kwa muda mrefu tangu nikiwa mdogo hadi sasa nimekuwa nikisikia hili suala lakini sifahamu hasasa sababu zake. Naomba kujua sababu za mtoto kuzuiwa asitoke nje ya nyumba hadi siku arobaini zipite. je ni sababu za kitaalam/afya, mila au dini? je kuna athari ama tatizo lolote akitoka kabla ya siku hizo?
 
mazoea hujenga tabia
kwa mama ndo kuna kuwa na tatizo kwa imani ninayoimani kwani anakuwa ni mchafu(nifasi}
 
ni uswahili tu ndo unatusumbua.hakuna sababu hasa za kisayansi.:A S-fire1:
 
Kwani wakati mtoto anachomwa sindano za chanjo anapelekwa hospitali bila kutolewa nje?
 
hizo ni imani tu wala hazina msingi wowote mbona mi kwangu nilimtoa wala hakuna kitu chochot
 
hizo ni imani tu wala hazina msingi wowote mbona mi kwangu nilimtoa wala hakuna kitu chochot

yaaah hata me nimejiuliza sana nikakosa jibu sababu hasa nini lakini wakina mama wengi kama si wote wanazingatia sana hili suala la siku arobaini lakini ukimuuliza sababu hana. Kwa upande penzi la mke baada ya kujifungua hilo halina shida sana kwa sababu maubile ya mama yanahitaji kujiweka sawa na uchafu kutoka mwilini hivyo hata akikaa zaidi ya siku arobaini ni sawa tu!
 
Back
Top Bottom