mtoto kutotembea

Hajto

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2013
Posts
5,646
Reaction score
5,606
jamani salama wapendwa,tatizo langu ni kuwa kuna mtoto wa kiume wa dada yangu kwasasa ana umri wa mwaka 1 na miezi kumi na mpaka sasa hajaweza kutembea....je tatizo litakuwa nini hapo wadau
 
Watoto wa kiume wanachelewa kutembea na kuongea sana ila almost miaka miwili hiyo ni tatzo...
Je lishe yake ilikua nzuri??
Je mnampatia vitu vya kumsaidia kutembea kama vile vibaiskel vya mbao vya miguu mitatu??
Je mmempeleka hospital??? Nini majibu ya daktari?
 
mkuu stany mzalendo, afya yake ni nzuri kabisa,na kibaskeli cha mbao anacho
 
mkuu stany mzalendo, afya yake ni nzuri kabisa,na kibaskeli cha mbao anacho

Umri wa watoto kutembea ni kati ya miezi nane na nusu mpaka miezi 20...kama mtoto hatembei baada ya miezi 20 tunasema amechelewa (Delayed Motor maturation)...mara nyingi sio tatizo kubwa maana kuna watoto wanachelewa kutembea kwa sababu hawajaona "umuhimu" wa kutembea yani hawana motivation...inawezekana wanaomzunguka hawampi sababu ya kutembea labda kwa kubebwa sana au mtoto kuletewa kila kitu kitandani kwa hiyo haoni sababu ya kuinuka maana yuko comfortable na position ya kukaa au kulala...unaweza kujaribu kumuwekea midoli mbali na alipo ili kumshawishi ainuke na kusimama ili afikie vivutio hivyo..

Kwasababu mtoto tunayemzungumzia amechelewa sana kutembea nakushauri umepeleke kwa daktari wa watoto ili achunguzwe zaidi kujua kama kuna tatizo kubwa ili tiba iwahi mapema ila kama hamna tatizo lolote basi usitie shaka maana utafiti unaonyesha hakuna tofauti ya ukuaji kiakili kati ya watoto wanaowahi kutembea na wanaochelewa maana mazingira ndio mara nyingi huchangia.

Siku njema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…