Mtoto wa Ali Kibao: Kama damu ya baba iliyomwagwa kikatili itakuwa chanzo cha majibu na mabadiliko basi atakuwa shujaa maradufu

Mtoto wa Ali Kibao: Kama damu ya baba iliyomwagwa kikatili itakuwa chanzo cha majibu na mabadiliko basi atakuwa shujaa maradufu

lugoda12

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
276
Reaction score
574
Anaandika Ali Kibao, mtoto wa kwanza wa mzee Ali Mohamed Kibao.
________

D68F9FD2-9D1E-4FD6-9E45-78A288142BB1.jpeg
Baba yetu hakutaka makuu wala umaarufu. Ali-dedicate sehemu kubwa ya maisha yake kwa wanawe na wajukuu zake. Hayo kwake yeye ndo ilikuwa fahari yake. Hata hivyo alikua mtu wa msimamo, mbishi sana na asiyeyumbishwa kirahisi.

Aliishi kwa principles na misimamo yake aliyojiwekea, na sasa wememuuwa, kitatili kabisa, kwa misimamo hiyohiyo. Haya ndo maisha tunayotaka kweli kama Watanzania? Sisi hatukudhani hata siku moja kama jambo hili linaweza kutotokea kwenye familia yetu. Tulikua tunaona habari (fulani katekwa, fulani kauawa) unadhani hayo ni ya wengine tu hayawezi kukufika na wewe. Haya, leo yametufika. Hakuna aliye salama.

Baba yetu alikuwa shujaa wetu. Lakini, kama damu yake, iliyomwagwa kikatili, itakuwa chanzo cha majibu na mabadiliko au itaepusha familia nyingine kupitia haya tunayoyapitia sisi, basi atakuwa shujaa maradufu (Rais wa zamani wa Msumbiji Armando Guebuza aliwahi kuandika "Your blood, yet more my blood, Shall irrigate our victory").

Baba amenifunza mengi sana, mengine niliyaelewa na mengine sikuyaelwa lakini naendelea kuyaelewa kadri siku zinavyokwenda. Baba yangu aligusa maisha ya watu wengi sana, na hakukata malipo yoyote kutoka kwao, kuanzia ndugu wa karibu, wa mbali na hata watu asiowajua.

Lakini pamoja na yote kuna watu wakapanga, sio wamteke tu, bali wamtese, waharibu mwili wake, wamuue, kisha wamtupe kama mbwa. Je kuna mwanadamu anayestahili kufanyiwa unyama kiasi hiki kweli?

Niachie hapa kwa sasa… 😭
 
Samia amehamishia TISS kwenye mamlaka yake moja kwa moja.

Damu za waliouawa na vyombo vilivyopo chini yake itatakwa mikononi mwake.

Hawezi kuzuia gadhabu ya Mungu dhidi yake na wahusika wote.

Tunajua TISS imejaa ruthless killers. Lakini siyo robots ni watu na watalipia hapahapa
 
Watalipa Tu HAKUNA namna Tena!
 
Back
Top Bottom