Mbu naona kidogo unatubabaisha akina mama. Huyo mtoto akisha zaliwa tu upewe unadhani ni mama gani mwenye akili zake timatu akupe mtoto wake mchanga? Utamnyonyesha na kumuhudumia ipasavyo kama mama mzazi? Na hapa sizungumzii kutafuta mfanyakazi ukamlipa fedha ili amhudumie wakati mama mwenyewe hayupo, au uwape dada zako au mama yako mzazi - never!
Unazungumzia uwezekano wa kupata surrogate mother akuzalie halafu akukabidhi mtoto ujue hiyo ni ngumu sana kwa kwetu Afrika.
Namba mbili, uwezekano wa kupata mtoto wa kike au wa kiume ni 50-50 kama alivyozungumzia mchangiji mmoja hapo juu. Upo uwezekano wa kuongeza chances za kupata mtoto wa kike lakini hiyo siyo guarantee. Jee akipatikana mwanamme ndiyo utamkataa?