Mtoto wa kiume kwasasa alindwe kama mtoto wa kike, maana hali sio hali

Hemedy Jr Junior

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2023
Posts
915
Reaction score
1,082
Wazazi mmekuwa bize sana walahi, imani ya kwamba mnawatafutia watoto wenu ili wasije kuteseka mnakosea sana maana mwenye uwezo huo ni Mwenyenzi Mungu pekee. Mnapamnana na bado hali ni ile ile, tumezaliwa ili tusaidiane.

Watoto wa kiume wamearibikiwa kwa sababu wazazi baadhi hawana hata hofu ya Mungu, malezi hawajui, wanajua kupika na kutandika kitanda basi. Inauma sana. Kila mtu amekuwa bize na kutafuta pesa.
 
Tuna jamii ya vijana wanaoaminishwa kupewa pewa hela na Kila kitu ndo mapenzi

Sasa wamejifunza wapi hili??ndo jibu lipo wazi malezi ya mzazi mmoja ambaye hana sura mbili..yeye ni soft tu kwanza ni Bank teller kupiga mtoto ni unyanyasi,mi mwanangu aguswi ,hujui uchungu wa uzazi wewe

Junior chukua hela kanunue ice cream, junior chukua hela kanunue chips mayai ya kisasa ule, watoto wana vimba makalio kwa hela za kupewa hovyo hovyo na wazazi wao kwa mwamfuli wa mapenzi a.k.a proudly single mom au my son my everything...

Sasa wanapokufa mama zao,au uchumi kuyumba basi vikina Junior ndo vinakutana na ukweli hela haitoki hovyo na kwakuwa vimejifunza kwa mzazi kwamba maisha ni kudanga na vina wajomba wengi ambao walikuwa wakija basi vinapakatwa na kupewa hela ya chocolate basi vinakuja na mindset ya mjomba ni mama huku vikisahau mjomba ana mashine

Basi mjomba anavipelekea miyooto...

Father figure ndo issue kubwa...mkubali mkatae watoto wakiume km ni lazima walelewe na mzazi mmoja kwa sababu yeyote ile ni bora walelewe na Baba.. Mwanamke hasa hawa modern woman hawana mabavu ya ku mtrain mtoto wa kiume kumuandaa na Maisha na uhalisia Wake...

Atakachofanya ni kumjaza matako,mashavu,kumyoa kiduku,kumpaka lotion makalioni na kupita nae akijivunia mwanangu mzuri mwanangu mzuri.. Makalio yakiongezeka anaanza kumsimanga unanenepa sana sahivi simununulia chips mayai...

Aina hiyo ya upendo haina msaada kwa mtoto wa kiume..shauri yenu
 
Umeongea point sana. Afu kingine Mzazi wa kike anadekeza mtoto sio kulea mtoto. mashoga wengi tunatengeneza ..au vibaka n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…