actually anayetuma msg siyo mwanamke. Mimi niliwasiliana naye hadi point ya mwisho. Ilipofikia kwenye kutuma hela akanambia nitume kwenye akaunti ya mchungaji wake ambaye alinipa jina na akaunti namba yake. Kwa madai yeye yupo kwenye kambi ya wakimbizi haruhusiwi kuwa na akaunti. Jina la mchungaji ni la kiume. Kwa hiyo inaonyesha kwamba huyo jamaa anazo picha za huyu mdada na anazitumia kwa ajili ya utapeli. Nilipopata lile jina nikaingia kwenye mtandao na kutafuta hiyo benk, nikakuta ni ya Nigeria. Nikaforward hilo jina polisi ya nigeria, hadi leo sijawahi kupata majibu.