SoC01 Mtoto wa maskini kusoma chuo kikuu bila mkopo

Stories of Change - 2021 Competition

Emanuel Chogo

New Member
Joined
Sep 8, 2021
Posts
2
Reaction score
2
Natumaini ndugu zangu wote wa jamii forum ni wazima wa afya ,Kwa ufupi nitaeleza stori ya kweli kuhusu Maisha ya kijana maskini chouni bila ya mkopo na fursa za kujiajiri

Naitwa Hiro nimezaliwa Tanzania katika jiji la Arusha wakati na zaliwa mama alikuwa anafanya kazi kiwanda cha nguo kinachoitwa Sunflag na baba kiwanda cha dawa, Ghafla nilpozaliwa tuu Baba akafariki nikiwa na miaka miwili hatujakaa sawa mama naye akaanza kuugua mapafu ikawa ndio safari yake ya kufanya kazi kiwandani ikaishia hapo tukarudi kijijini Manyara

Elimu ya chou kikuu bila mkopo

Mwaka 2018 nilibahatika kupangiwa chou kikuu cha Dodoma katika kitivo cha Sayansi na technolojia kusomea degree ya IT nilifika chuoni japokuwa sikuwa na mkopo ,niliamini nitapata mkopo nikafuatilia bachi zote sikupata mkopo nikawaza nirudi nyumbani, nikakumbuka nilikuwa nalipwa elfu hamsini kwa mwezi nilipomamliza kidato cha nne, nikasema hata nikirudi sitaweza kujilipia ada ya milioni moja na lakitano kwa mwezi , baadaye nikaomba watu mbali mbali angalau nipate laki tano nifanye usajili wa muda yaani partial registration kwa sababu nilikuwa sijapata chumba kwenye hosteli ,nikamalizia usajili wa muda mfupi kwa kulipa laki tano katika miloni moja na laki tano .Maisha yakawa magumu sana ndio mara ya kwanza kulala njaa nikiwa chou kikuu nikawaza nitakula nini ? nikaomba sana nikasali sana lakini wakati wa Mungu ulikuwa bado haujafika kila nikienda bodi ya mkopo naviambatanisho vyote cheti cha kifo cha baba na barua ya kaya maskini zinazosaidiwa na Tasafu lakini sikupata msaada Zaidi ya kupewa majibu subiri batch zinazokuja, nilijiskia vibaya sana ndipo nikajua mvua za Dodoma huwa zinanyesha dakika yeyote na kukatika hapo hapo na jua la Dodoma linawaka wakati wowote nakumbuka siku moja nilikuwa naenda bodi ya mkopo nikiwa na matumaini ya kufanikiwa ghafla nikiwa kituo cha kupandia daladala mvua ikanyesha nikaloana nikajipa moyo nikapanda daladala nilipofika bodi ya mkopo wakaniambia utawala mkuu ndio unatakiwa utume taarifa zangu bodi ya mikopo. Nikapanda daladala kuelekea utawala mkuu nikashuka kituo cha daladala ghafla mara ya pili hali ya hewa ikabadilika mvua ikaanza kunyesha amini usiamini wenye magari yao walinipita japo nanyeshewa na mvua sikukataa tamaa nilikaa nje mpaka nikakauka kisha nikaingia utawala mkuu na kuwaomba watume taarifa zangu wakanihakikishia mambo yapo sawa nikarudi nikiaminini nitapata mkopo .Muhula wa pili ukaisha bila ya kupata mkopo nikiwa na deni la milioni moja nikaenda field bahati nzuri ilikuwa ni chouni. Nikaamua kukopa wanafunzi wenzangu nakuanza kufanya biashara ya uwakala yaani m-pesa,tigo pesa na eartel money eneo la nane nane

Matokeo yamwaka wakwanza yakatoka yalikuwa mabaya sana kwani nilikuwa na supplementary mbili baada ya kuyaangalia yakafungiwa kwasababu nilifanya usajili wa mda inatakiwa nilipe mlioni moja ndipo yafunguliwe nikarudi nyumbani, mama hafanyi kazi yeyote tangu aache kazi kiwanda cha nguo nikamweleza akaniambia twende kwa shimeji yangu nikamuombe nikamwambia sizani kama atakubali akanilazimisha hatimae nikakubali lakini huyu Mungu hujibu watu kupitia watu akakubali kunisaidia milion moja wakati huo nimeshaomba mkopo mwaka wa pili nikaenda chou nikalipa deni kwa bahati mbaya wakati nalipa lile deni nikalipia kwenye control namba ya mwaka wa pili nilipomwelezea muhasibu akaniambia hamna shida ntaifanyia transfer kwenda mwaka wa kwanza ili ufanye malipo ya mwaka wa pili

Nikaenda kwa mkuu wa department kumwelezea alipo angalia kwenye system ya malipo akaniambia mbona unadaiwa hela ya hostel tu ada umeshalipa kumbe muhasibu hakufanyia transfer ile hela niliyolipa kwenye control namba ya mwaka wa pili nilimpa jibu moja sawa nitalipia ,nikalipia hostel kabla muhasibu hajafanya transfer na kukamilisha usajili.

Nikazidi kusali bila mafanikio nikakata tamaa maana sina pesa ya kula wala sina namna ya kupata pesa nikaacha kusali siku moja Rafiki yangu akanipitia akiwa anaenda kanisani na kuniambia twende kanisani nikakubali tukaenda kanisani wakati wa mahubiri mchungaji akasema kuna watu wanamatatizo ya kutopata watoto kwa mda mrefu kisha wakapita mbele kila mmoja akaanza kutaja miaka ya ndoa yake wengine kumi,ishirini cha kushangaza na mchungaji naye Zaidi ya miaka 30 katika ndoa yake hajapata mtoto na ameombea wengi wamepata Watoto na bado anaamini atapata mtoto nilijiskia aibu sana kwa jinsi nilivomuomba Mungu nipate mkopo kwa mwaka mmoja kisha nikakaa mbali na Mungu kwasababu hajanijibu

Matokeo ya mwaka wa pili yakatoka ila yalifungiwa kwa sababu nadaiwa ada nikawaza ntapatia wapi hiyo pesa nikapambana nikapata kwa kuomba omba nikaenda kulipia matokeo yalipotoka ikaonekana nimmedisco nililia sana nikaamua kupangisha njee ya chuo nikilia mchana na usiku , kisha nikakata rufaa ya matokeo mwezi wa kumi na mbili .Ghafla nikapata taarifa kutoka bodi ya mikopo wamenipa mkopo wakati huo huo kwenye matokeo inaonekana nimmedisco nikagubikwa na mshangao maana naona nikenda kulia kama dunia inaenda kushoto

Baadae nilishinda kesi matokeo yakawekwa na discontinue ikaondolewa nikafanya mitihani ya muhula wa kwanza mwaka wa tatu matokeo yakatoka nikawa nimepata supplementary moja kwasababu sikupresent project kutokana na changamoto ya kufuatilia rufaa nilienda kuongea na mkuu wa department alinipa jibu liliniumiza moyo utarudia mwaka hautaweza kumaliza mwaka huu kufanya project, nilijaribu kumweleza yaliyonikuta lakini hakunisikiliza nikafanya mitihani ya muhula wa pili baadae niliamua kumuachia Mungu lakini mkuu wa department alikubali na nikamaliza chuo

Hitimisho:

Nawashauri bodi ya mikopo wawaangalie vizuri hao walengwa ambao wamesema watawapa vipao mbele wajiulize inakuaje wana matawi Tanzania nzima na vyuoni kunamtu hana baba wala mama na hana mkopo na wanaenda mpaka kwenye ofisi zao hawapati mikopo ,naumia sana haswa wengine ni Watoto wakike matokeo yake wanajiingiza kwenye ulevi ili kuondoa mawazo kutokana na Maisha kuwa magumu ,wengine wanafanya biashara za kujiuza (na mengi ya kuelezea kwenye biashara ya kujiuza kwasababu inasikitisha sana ,hadi vijana wakiume wanajiingiza kwenye ushogo) mwisho wanapata maradhi kama UKIMWI au anapata mimba , ni lini bodi ya mikopo wameenda vyuoni wakauliza ninani ambaye hana baba wala mama na nimlemavu hajapata mkopo lakini utasikia kila mwaka bodi ya mikopo imeongeza asilimia ya wanufaika wa mikopo na wanaoumia ni wengi ndoto za wengi zimezimwa na bodi ya mikopo wanalia usiku na mchana jua likiwapiga na mvua ikiwanyeshea bila mafanikio

Pia nilijifunza fursa zifuatazo ambazo kijana anaweza kufanya na ikamwingizia kipato tofauti na kuajiriwa maana manyanyaso ni mengi Zaidi boss atakuuliza wateja wako wapi

  • Namba moja nikumuamini Mungu ,ili uwe na Moyo shupavu na wenye ujasiri muamini Mungu pambana yeye atafungua njia na atakupa connection
  • Kazi ya kuuza vyuma chakavu na mifuko ambayo nilikuwa naifanya nilipokuwa shule ya msingi ,ni fursa nzuri kwa vyuma chakavu ambavyo vinapatikana kwenye gereji na mitaani na mifuko utauzia sehemu mbali mbali kama kwenye minada na sokoni
  • Kuwa dalali kwa kutumia social media kama WhatsApp,Instagram na facebook niliweza kufanya biashara ya kuunza laptop kwa wanafunzi,viwanja,vyumba vya kupanga na vitu vya ndani kama kitanda ,meza
  • Kufanya kazi ya kuwa wakala ,ni miongoni mwakazi ambayo itakuingizia kipato kama utakuwa na mtaji na eneo zuri lenye watu wengi kama stendi na sokoni
  • Pia nilipokuwa stendi niliona watu wamejiongeza kwenye fursa nyingi kama zifuatavyo:-
  • Kubeba mizigo; wengi walikuwa wakibeba mzigo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine si chini ya shilingi miatano
  • Kukatisha tiketi,nilikutana na watu amabao wamesoma na wanaelimu za juu lakini Maisha yao yamekuwa mazuri kwa ajili ya kukatisha tiketi na wanafamilia zinazowategemea kwasababu kwa abiria mmoja mtu anapata si chini ya elfu mbili
  • Kuunza maji,biskuti,vifaa vya electronic kama earphone,chaji,soda ni bidhaa ambazo abiria wanazipenda
  • Kuwa na ufundi mfano mimi ni fundi wa laptop na simu pia nilipokuwa nafanya kazi stendi niliona watu wanaendesha familia kwa kushona vyatu vya wat
  • Pia biashara ya kuuza magazeti ,nakumbuka mwaka 2015 baada ya kumaliza kidato cha nne nilianza kuuza magazeti kila gazeti la shilingi elfu moja unapata faida ya mia hamsini na gazeti la mia tano faida ya hamsi mpaka kufika jioni najikuta nimeingiza Zaidi ya shilingi elfu tano
  • Pia biashara kuuza vyungo mbali mbali vya chai kama mdalasini,karafuu,tangawizi ni bidhaa ambazo pia hutumika kama dawa na hutumika kila siku majumbani ni rahisi sana kumshawishi mteja achukue
  • Pia niliona fursa ya Saloon walioanzisha na waliojifunza kunyoa na kusuka ilikuwa fursa kubwa mfano mzuri nilipoona nimedisco nikapangisha karibu na chuo kunamdada ni mhitimu amejifunza ususi hana ofisi lakini kwenye hicho hicho chumba chake ndo anawasuka wanafunzi kwa siku anaingiza Zaidi ya elfu hamsini
  • Pia biashara ya kupaka rangi kucha ni biashara ambayo inafaida kubwa kama utakuwa na umakini kwasababu kumpaka mtu mmoja rangi ni elfu tatu jiulize kuanzia asubuhi mpaka jioni unashingapi kwa Dodoma tembelea Nyerere square utajifunza kitu
  • Pia biashara ya kupiga picha, ni moja ya biashara ambayo inahitaji uwe na kamera lakini ukiwa mwepesi unaweza kufanya bila ya kuwa na camera mfano Dodoma eneo la Nyerere square unaweza kumtafuta mteja na kuazima camera ni eneo ambalo watu wengi wanapapenda kwaajili ya mandhari nzuri ya kupigia picha
  • Pia biashara ya kuuza matunda ndizi,machungwa,nanasi,parachichi na maembe mfano ndizi Rafiki yangu anauza ndizi stendi ya sabasaba Dodoma bei ya jumla anachukua kuanzia shilingi hamsini yeye anauza mpaka mia mbili na kwa siku anauwezo wa kuuza ndizi kuanzi miatatu ukizidisha mara hamsini ni faida ya kutosha
  • Pia biashara ya kuuza mishkaki na kuuza chipsi
  • Biashara ya kuuza juice na ice cream
  • Biashara ya kuuza urembo , ni moja ya biashara ambayo nilijaribu kuifanya nilipokuwa chuo mwaka wa pili kwasababu nilingundua wanawake wa rika zote wanavaa urembo kama hereni
fffffffffffffff6�~A%4%
 
Upvote 3

Daah ni muujizaa !!!mshukuru Mungu Sana
 
Back
Top Bottom