DOKEZO Mtoto wa Miaka 10 ameajiriwa kazi za nyumbani Kimara Stop Over, ananyanyaswa sana, Waziri Gwajima msaada wako unahitajika

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hapa mtaani kuna mama mmoja anaitwa Mama Nancy amemuajiri mtoto ambaye kwa umri sina uhakika lakini nahisi ana umri wa miaka 9 au 10, ameajiriwa kama house girl.

Kibaya zaidi Mama Nancy amekuwa akimnyanyasa huyo mtoto, anampiga anamfokea na inadaiwa amemkataza kuzungumza na watu wengine nje ya familia yake ili wasije wakamfungua akili.

Mtoto huyo amekuwa akiishi kinyonge muda mwingi, anapata mateso makali tena ya waziwazi ambayo sisi majirani tunaona, vipi kuhusu yale ambayo hatuyaoni yanayofanyika kwa ndani?

Mtaa unaoishi na ambao ndio mhusika huyo anapatikana unaitwa Umoja Street, ni Kimara Stop Over (Dar es Salaam).

Mtu ambaye anataka kushuhudia au kama Serikali inataka kufuatilia, wakifika hapo Stop Over, waulizie kwa Dereva Bodaboda kuwa wawapeleke Mtaa wa Dkt. Kayuni au Kanisa la Mabati.

Wakifika hapo nyumba hiyo ina geti la jeusi, chumba cha kwanza cha wapangaji, ndipo anaposhi mama huyo.

Mama huyo ni Mwalimu, anafundisha Shule ya Msingi ipo mitaa hiyohiyo ya Kimara.

Mtoto huyo ameajiriwa hapo wiki za hivi karibuni, ametokea nje ya Dar, aliyemleta ni mama mmoja (rafiki wa Mama Nancy) ambaye kazi yake anachukua Watoto wadogowadogo kama huyo house girl kisha anawabebesha bidhaa wauze mtaani, bidhaa kubwa anayowabebesha ni sabuni.

Mimi nazungumza kwa kuwa natarajia kuwa mzazi, hivyo ninapoona Mtoto mdogo kama huyo anafanyia hayo inamanisha nami Mtoto wangu ipo siku anaweza kufanyiwa kama hayo.

Mama Nancy ambaye ni mama wa Watoto wawili, anaonesha roho mbaya kiasi kwamba ni kama hana Watoto.

Naomba Waziri Gwajima kupitia Wizara yake amsaidie mtoto huyu pamoja na Watoto wengine wote wanaotolewa mkoani na rafiki wa mama Nancy kisha kuja mjini kutumikishwa.

Inawezekana wazazi wa Watoto hao ni masikini n ndio maana wanawaruhusu Watoto wao waje mjini bila kujua wanachopitia.
 
Kama kweli haya uyasemayo mnayaona maanayake mtaa mzima ama majirani wote mnamuogopa huto mama nacy right..🤔
Yaani hata balozi hakuna hapo mtaani kwenu mkuu...!!

Kwani mmeshindwa kumshiraki huyo mama nancy hata basi kwa mwenyekiti wa mtaa..??

Anyways, sijui namna ninavyo litazama hili jambo mimi kama mzazi ningekua nimesha chukua hatua hata kabla, na kisha ningekuja hapa jamvini kulitolea taarifa ili wahusika waweze endelea na hatua stahiki
 
Ujumbe umefika! Dkt. Gwajima hatakawia kufuatilia.
 
Watu wengi ni wabinafsi?. Hawajali kinachowapata wengine maadam wao hawaathiriki. Alichofanya mdau kutoa taarifa ni cha kiungwana. Anastahili pongezi.
 
Anzia serikali ya mtaani kwako na acha umbea kuingilia nyumba za watu. Muache aendelee kumtesa au uchukue huyo mtoto uishi nae kwako umlee vile unavyoona wewe inafaa.

Watoto wa mitaani watapngezeka Kwa serikali hii ya ccm.
Hajaingilia nyumba za watu. Ametoa tu taarifa ya alichokishuhudia ili wenye mamlaka wachukue hatua stahiki.
 
Asilimia zaidi ya 70% ya hii vita ni propanda.

Asilimia 30% zilizobaki ni hatua kali za kisheria na mikakati ya social services in coordination na wizara.

Hiyo sio vita ya dorothy Gwajima peke yake.

Hayo mambo yanataka 30% mikakati ya local government initiatives na story yenyewe ni ndefu.

Hii vita Dorothy uwezi shinda dada yangu bila ya kusoma modules nilizokupa inataka committed inter professional team working ya idara kadhaa and high investment in propaganda.

Hao watu wengine awapo committed kupambana na hiyo vita ndio maana tuko hapa.
 
Andika kwa kiswahili hayo maneno uliyoyaandika kwa kiingereza ili kutoa uwanda mpana wa uelewekaji.Usiandike kama JF ni jopo la maprofesa wanajadili namna ya kuchenjua makinikia ya Buzwagi.Wigwa Mwanamalundi?😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…