CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,296
- 12,972
Habari yako charminglady
Je hali hii imeanza hivi karibuni au alikuwa nayo tangia awali?Je anakula kirejareja( mfano snacks)?Anatumia vyakula vyenye sukari nyingi kama chocolates au vinywaji vya sukari kama soda kabla ya mlo?Anapata choo mara ngapi kwa siku?
Sikushauri umpe mtoto dawa kwasababu amegoma kula.Kila mtu ana hamu tofauti ya chakula na mara nyingi sisi wakubwa tunaona watoto hawali chakula cha kutosha lakini hiko chakula anachokula kinamtosheleza kutokana mwili wake na mahitaji ya mwili.Kama ameshazoea kula mlo mdogo itachukua muda mpaka aweze kula mlo mkubwa kwasababu jinsi unavyokula chakula kingi ndivyo jinsi utumbo wako unavyoongeza capacity ya kubeba hiko chakula(unatanuka kwa lugha nzuri).
Nakushauri uwe unamshirikisha katika kuchagua mlo na ikiwezekane akusaidie kuutayarisha huo mlo,unakuwa unamtayarisha pshycolocially kwaajili ya huo mlo na anakuwa excited kwasababu anakula kile kitu ambacho anapendelea na amekitayarisha!
Unaweza kunijuza ana uzito kiasi gani na ni jinsia gani?Habari yangu njema.... Kwanza huwa hapendi vitu vya sukari, hivyo hatumii choclate wala soda.....
Yaan anakula chakula kidogo mno na ndivyo alivyo tangu kuzaliwa!! ukitaka kumpa adhabu mwambie ale chakula atalia mpaka macho yawe mekundu kisa hataki kula!!!
Unaweza kunijuza ana uzito kiasi gani na ni jinsia gani?
Average bodyweight ya mtoto wa miaka 10 wa kike ni approximately kilo 34
Minimum weight ni 25 kg,kwa maana hio akiwa chini ya kilo 25 atakuwa underweight,inamaana hapati chakula/virutubisho vya kutosha mwilini.
Maximum weight ni 51 kg,akizidi kilo 51 ni overweight!
Nakushauri umpeleke hospitali kama ana uzito wa chini ya kilo 25!
Naona hapo juu umeamua kwenda hospitali, ni vyema ukasikiliza ya huko kwa sasa!
Mtoto saiv anakula vizuri?Thanks daddito...... :smile:
Nilikuwa nasoma ushauri wako...kesho nitarudi nami hapa kutia dodoso.
Mtoto saiv anakula vizuri?
Uzito wake ulipata upo vizuri kiumri na urefu?
Mkuu, alifanyiwa body check up hakuwa na tatizo lolote. Uzito uko vizuri kiasi ila natamani sana apate hamu ya kula. Bado ni shida, njia mbadala tafadhali!