Mtoto wa miaka 12 amejiteka akiwa na mdogo wake huko jijini Mwanza!

Mtoto wa miaka 12 amejiteka akiwa na mdogo wake huko jijini Mwanza!

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643
#HABARI Katika hali isiyo ya kawaida mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina Frola Samson (12), mkazi wa wilaya ya Ilemela amepatikana baada ya msako wa Jeshi la polisi Mkoani Mwanza akiwa eneo la Buhongwa ambako alijificha yeye na mdogo wake aitwaye France Samson (8) huku akidanganya kuwa wametekwa na kutaka wazazi watume fedha ili waachiwe.

Inadaiwa kuwa watoto hao walitoweka nyumbani mnamo tarehe 4.7.2024, ambapo Frola aliiba pesa za Mama yake kiasi cha shilingi 150,000/= na kisha kutoweka na mdogo wake wakielekea Buhongwa ambako alianza kupiga simu kwa Mama yake mzazi akidai atumiwe pesa kwa ajili ya waliowateka ili wawaachie huru.

Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoani humo baada ya kupokea taarifa na kufanya ufuatiliaji, limefanikiwa kuwapata watoto hao wakiwa salama huku wakiwa na simu, godoro na vyombo vingine vya matumizi ya ndani walivyonunua kwa kutumia pesa aliyoiba mtoto huyo.

#EastAfricaTV

FB_IMG_1720272186182.jpg
 
Watoto wa siku hizi wanakua haraka sana kiakili hakyaMungu

nakumbuka mimi nimeanza kuuona utamu wa simu nikiwa kidato cha nne nikiwa na miaka 19

leo hii kitoto cha miaka 12 kinajiteka, kinapanga chumba kinalipa kodi, kinajipikia na kinaishi na mtu kama mtegemezi wake kabisa wakati kuna mababa mazima 30yrs yanaogopa kuoa huku yana ajira😅😅😅😂😂

Ogopa sana utandawazi
 
M
Mtoto anaona fedha za mama ni za mikopo kausha damu na vikoba vyao achilia mbali michango ya sherehe zisizoisha kwenye vikundi vyao huku nyumbani mahitaji ni 0:0.

Dogo kaona hapa nisimuache mdogo wangu,atakufa kwa njaa,ni bora niondoke naye nitapambana ale nami nile ili nimuoneshe mama namna ya kuwajibika kama mzazi.

Huyo dogo siyo tapeli ndio maana fedha alizohamisha kanunulia mahitaji ya msingi,asaidiwe bila kupingwa.
 
Kama hakuna mtu nyuma ya pazia basi huyo Flora atakuwa anauwezo mkubwa sana wa akili.

Pia yawezekana labda hapo nyumbani maisha wanayoishi ni ya mateso ndio sababu akaamua kutumia mbinu ya kutoroka yeye na mdogo wake ili kukimbia manyanyaso na mateso. Maana kwa hali ya kawaida kama familia wazazi wanaishi vizuri na watoto na wanaupendo na mahaitaji wanapata ni nadra kutokea hii kitu.

Scenario zote mbili ya kuwa kuna mtu mzima anahusika au hii ya kukimbia mateso zinawezekana. Ukweli mimi sijui nimejaribu kuwaza tu nje ya box.

Watoto wahojiwe tuufahamu ukweli. Tusikimbilie kuhukumua kuwa "amejiteka na kuiba hela".
 
Katika hali isiyo ya kawaida mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina Frola Samson (12), mkazi wa wilaya ya Ilemela amepatikana baada ya msako wa Jeshi la polisi Mkoani Mwanza akiwa eneo la Buhongwa ambako alijificha yeye na mdogo wake aitwaye France Samson (8) huku akidanganya kuwa wametekwa na kutaka wazazi watume fedha ili waachiwe.

Inadaiwa kuwa watoto hao walitoweka nyumbani mnamo tarehe 4.7.2024, ambapo Frola aliiba pesa za Mama yake kiasi cha shilingi 150,000/= na kisha kutoweka na mdogo wake wakielekea Buhongwa ambako alianza kupiga simu kwa Mama yake mzazi akidai atumiwe pesa kwa ajili ya waliowateka ili wawaachie huru.

Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoani humo baada ya kupokea taarifa na kufanya ufuatiliaji, limefanikiwa kuwapata watoto hao wakiwa salama huku wakiwa na simu, godoro na vyombo vingine vya matumizi ya ndani walivyonunua kwa kutumia pesa aliyoiba mtoto huyo.

East Africa

FB_IMG_1720275993652.jpg
 
Back
Top Bottom