Mtoto wa miezi 4 kukohoa na kulia sana usiku shida ni nini

Mtoto wa miezi 4 kukohoa na kulia sana usiku shida ni nini

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Mtoto wa miezi 4 analia sana usiku amechoma sindano wiki 2 zimeisha tumempa amoxilin wapi nasasa tumempa sefalexin kikohozi bado kinaendelea
Juu ya yote Analia sana usiku kwa kushtuka kila baada ya dk arobain anashtuka na kuanza kulia anabembelezwa akishtuka naanza kulia hii hali Sasa ni zaidi ya wiki ya tatu Sasa shida ninini?

Madaktari naomba msaada wenu asanteni
 
Hawawezi kujua kirahisi mkuu, nakushauri kwa tatizo kama hilo nenda kafanye vipimo. Pole sana ndugu
 
Mtoto wa miezi 4 analia sana usiku amechoma sindano wiki 2 zimeisha tumempa amoxilin wapi nasasa tumempa sefalexin kikohozi bado kinaendelea
Juu ya yote Analia sana usiku kwa kushtuka kila baada ya dk arobain anashtuka na kuanza kulia anabembelezwa akishtuka naanza kulia hii hali Sasa ni zaidi ya wiki ya tatu Sasa shida ninini?

Madaktari naomba msaada wenu asanteni
Moderators heading isomeke kukohoa na c kukomoa nimeedit heading haina option ya kuedit
 
Kuna dawa ya mitishamba iko packed well na inauzwa pharmacy ina box la njano aiseeehhh ni nzuri, mwanangu alikohoa tangu January ila majuzi nikampatia hiyo dawa mambo yakawa safi
 
Kuna dawa ya mitishamba iko packed well na inauzwa pharmacy ina box la njano aiseeehhh ni nzuri, mwanangu alikohoa tangu January ila majuzi nikampatia hiyo dawa mambo yakawa safi
inaitwaje
 
Mtoto wa miezi 4 analia sana usiku amechoma sindano wiki 2 zimeisha tumempa amoxilin wapi nasasa tumempa sefalexin kikohozi bado kinaendelea
Juu ya yote Analia sana usiku kwa kushtuka kila baada ya dk arobain anashtuka na kuanza kulia anabembelezwa akishtuka naanza kulia hii hali Sasa ni zaidi ya wiki ya tatu Sasa shida ninini?

Madaktari naomba msaada wenu asanteni
Sababu 6 Zinazofanya Mtoto Mchanga Kulia Usiku


Kwa mzazi yeyote anaelewa usumbufu unaotokana na mtoto anaelia. Watoto wachanga wenye umri chini yua miezi 6 wanakuwa na matatizo haya zaidi.

Mtoto anapolia huwa inaleta hisia kuwa mtoto anashida na mara nyingi wazazi au walezi wanakuwa hawajui sababu au hata wakijua huenda wasijue jinsi ya kurekebisha tatizo na kumnyamazisha mtoto.

Ifahamike kwamba kulia ndio njia pekee ambayo mtoto anaitumia kuwasiliana na wengine juu ya shida ambayo anayo. Ni ujumbe kwa mzazi au mlezi kuwa hajisikii vizuri na anahitaji msaada.

Kwanini mtoto mchanga huwa analia? Soma sababu sita kubwa zinazomfamnya mtoto mchanga kulia na mbinu za kumnyamazisha. Namba sita ni muhimu kuijua kwa undani kwakuwa ndiyo inayosumbua wengi zaidi.

Sababu 6 Kubwa za Mtoto Mchanga Kulia Usiku
1. Njaa
Mtoto akiwa na njaa na anahitaji chakula anaweza kulia ili kutaka shida yake itatuliwe. Lakini kwa bahati mbaya hana namna ya kukujulisha kuwa ana njaa zaidi ya kilio. Ni vyema kufahamu aina ya sauti ya kilio inayoashiria njaa. utajua hili kwa mazoea yako ya kila siku na mtoto wako. Njaa ni mojawapo ya sababu kubwa kabisa ya mtoto mchanga kulia.

Njia ya Kukabili Tatizo:

Mpe mtoto chakula kila mara kutokana na ulivyompangia. Kumbuka mtoto anakula kidogo na mara kwa mara.

Kama mtoto anaendelea kulia baada ya kula au anakataa chakula basi kutakuwa na sababu nyingine

2. Joto au Baridi
Kama ilivyo kwa watu wazima,joto kali kupita kiasi au baridi inakufanya ujisikie vibaya na kutafuta jinsi ya kurekebisha kama vile kuvaa vazi zito kama kuna baridi au kuwasha feni au kiyoyozi,vivyo hivyo kwa mtoto mchanga, anahitaji kupata ubaridi kama kuna joto kali au kuvikwa nguo nzito ili apate joto kama kuna baridi


Njia ya Kukabiri Tatizo:

Hakikisha mtoto anavaa nguo sahihi kulingana na hali ya hewa. Mpunguzie nguo au kufungua madirisha kama kuna hali ya joto.

Kama kuna baridi basi hakikisha unamvikanguo nzito mwilini ikiwemo miguuni na kichwani.

3. Uchovu na Usingizi
Watoto wanalia wakiwa na usingizi. Hii inatokea mara nyingi sana. Watoto wengi wana tabia ya kulia kabla ya kulala.

Njia ya Kukabiri Tatizo:

Fahamu kuwa mtoto anahitaji kulala muda mwingi sana inakadiriwa kuwa masaa yapatayo

Mtoto wa miezi 1-3: Masaa 15 (Mchana-5,Usiku-10)

Mtoto wa miezi 3-6: Masaa 14 (Mchana-4,Usiku-10)

Mtoto wa miezi 6-13: Masaa 12-14 (Mchana-3,Usiku-11)

Kama ukifahamu mtoto analia kwasababu ya usingizi au uchovu basi muogeshe na kumweka katika mazingira ya kulala(kumlaza mtoto)

Watoto wengine wanalala vizuri wakiwa wameshikwa mikononi na kuchezeshwa badala ya kitandani.

4. Kubebwa na Kukumbatiwa
Watoto wanahitaji kubebwa na kukumbatiwa. Hii ni njia yaasili ya kunesha upendo kwa binadamu huyu mdogo.

Njia ya Kukabiri Tatizo:

Mtoto anapokuwa amelazwa kwa muda mrefu huwa anachoka na anahitaji kumbadirisha namna ya kulala napengine kubebwa mikononi na kukumbatiwa. Sauti ya mapigo ya moyo ukimbeba kifuani kwako inamfanya ajisikie vizuri na kujiona anajaliwa.

5. Kubadirishwa Nepi
Mtoto anapojisaidia katika nguo zake anajisikia vibaya na kukosa uhuru.

Anahitaji kubadirishwa nepi,kuoshwa na kuvikwa upya

Mtoto akilia fikiria huenda amejisaidia na anahitaji kubadirisha nepi

Njia ya Kukabiri Tatizo:

Mwangalie mtoto mara kwa mara kama amejisaidia na mbadirishe nepi zilizochafuka. Nepi zenhye mkojo au haja kubwa zinaweza kumsababishia mtoto kuungua ngozi hivyo ziondolewe kwa haraka.

6. Ugonjwa wa Tumbo na Maumivu Mengine
Watoto wachanga wanasumbuliwa sana na maumivu ya tumbo na wataalamu wanasema kuwa inaweza kusababishwa na chakula ambacho katika umri mchanga ni mziwa ya mama au maziwa ya bandia ambayo anapewa.

Kwakuwa mfumo wake wa chakula bado ni mpya na unaendelea kukua basi unapata shida kumeng’enya chakula.

Inaaminika kuwa gesi inajaza tumbo na kusababisha maumivu kwa mtoto.

Njia ya Kukabiri Tatizo:

Shida hii si rahisi kukabiliana nayo na imekuwa ikiwapa wakati mgumu wazazi kwa watoto chini ya miezi 3.

Kumlaza mtoto kifudifudi iliatoe upepo ni njia mojawapo inayoshauriwa lakini katika usimamizi(Ni hatari kumlaza mtoto mchanga kifudifudi kwa kuwa anaweza akajiziba hewa na kusababisha kifo).

Kumshikashika tumbo kwa mikono au kitambaa chenye maji ya uvuguvugu inaweza ikasaidia kumtuliza.

Kuna dawa za kusaidia kulainisha utumbo wa mtoto na kutoa gesi. Tafadhari onana na daktari wa watoto upate ushauri zaidi.

Mwisho..
Mtoto anaelia anahitaji msaada na anatoa mawasiliano kuwa ana shida. Kwakuwa hawezi kusema wala kuonesha ni nini unahitaji kuangalia mambo yote ya msingi kama yalivyotajwa ilikujua anasumbuliwa na nini.

Ugonjwa tumbo unachangamoto kubwa zaidi kukabiliana nao na kwa kweli unawasumbua watoto wengi na wazazi pia kwa kuwa hakuna kikubwa ambacho uaweza kufanya kuondoa maumivu kwa mtoto wako. Hata hivyo bado mbinu zilizotajwa zinaweza kusaidia kukabiriana na matatizo yanayosababisha mtoto mchanga kulia usiku.

Tueleze changamoto unazozipata juu ya mtoto wako mchanga kulia usiku. Unatumia mbinu zipi na unafanikiwa kwa kiwango gani? Shiriki kwa kuandika katika kisanduku cha maoni hapa chini.
chanzo.Sababu 6 Zinazofanya Mtoto Mchanga Kulia Usiku
 
Asante mkuu Nilimpima akaonekana Ana Naimonia Sasa sindano zote hizo hajapona Why
Mkuu mpeleke mtoto hospital,nimeshuhudia mtoto akianga dunia kisa Pheunimonia. Siyo nzuri kbs...tena kama upo naye nyumbani bado mkimbize hospital...mwenyewe mwanangu aliumwa hii kitu ila niliitibu haswaa. Mara nyingine uwa wanaongeza dose wakiona bado inamsumbua.

Kinachomfanya kulia ni kukosa pumzi kutokana na maumivu mapafuni inayompelekea kushindwa kupumua vema. Ndyo maana ukimsikiliza akiwa anapumua unasikia kama vimilio flan hivi...na kukohoa ni stage ya ugonjwa kukomaa,mwisho wa siku utakuta hadi mafua yanatoka na rangi ya kijani...nakuomba chukuwa hatua haraka.
 
Back
Top Bottom