Mtoto wa mwezi mmoja (siku 30) kutopata choo

Edward Chapa

Member
Joined
Jun 30, 2012
Posts
72
Reaction score
12
Habayi za Mapumziko ndugu, poleni na majukumu.
Mimi ni baba wa mtoto wa kike wa umri wa siku 30 ( mwezi mmoja) hajapata choo leo ni siku ya 7 (wiki),na anatumia maziwa ya mama.
Tatizo nini??
Nimpatie dawa gani??
Naombeni ushauri ,sababu napatwa na presha.
 
Kawaida sana, kama halii na ananyonya kawaida, there is nothing to worry edo, endelea tu kumshukuru Mungu kwa kukubariki na hako kabinti 🙂
 
Kawaida sana, kama halii na ananyonya kawaida, there is nothing to worry edo, endelea tu kumshukuru Mungu kwa kukubariki na hako kabinti 🙂

Asante ndugu, namuomba Mungu azidi kumbariki akue kihekima na kimo
 
Ukiona hivyo ujue maziwa ya mama yanafanya kazi vizuri kukuza mwili wamtoto,
hata usiogope ni jambo la kawaida
 
Atapata baada ya siku ngapi??
 
Edward acha kusikiliza watu wasiojua kitu. Inshort mtoto akikosa choo kwa zaidi ya siku 7 ni tatizo(abnormal), hivyo unatakiwa umpeleke hospitali mapema sana. Kuna uwezekano utmbo ukawa umejikunja ingawa sio lazima iwe. Cha kuogopa zaidi ni kama akipata intestinal obstruction ambapo anaweza akahitaji upasuaji. Kwa hiyo kabla ya kujiridhina ni bora umpeleke hospitali mapema.
 
Asante nimekuelewa ndugu!
 
Asante kwa ushauri ndugu
 
siku atakaposhusha mzigo huyo...tani saba...nway,just jokin.ongea na dr wako tafadhali kwa ushauri wa kitaalam
 
mkuu pamoja na ushauri wa watu wengine, hiyo ni hali ya kawaida hasa kama hasumbui (hasa kujinyonganyonga sehemu za kiwiliwili) atapata tu choo! lakini ni vema kumuona specialist amtazamie kabisa, manake sisi wengi tuongea kwa experience tu!
 
Asante ndugu! Hasumbui wala hajinyonginyongi sehemu za mwili!
 
Nasikia kuna mtu ameniambia kuna dawa inaitwa mafuta ya samaki nimpatie, je kuna dawa kama hiyo kwa mtoto wa 30 days naona kama ni hatari??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…