Mtoto wa mwisho hafai kuoa?

wanafaa sana tu kuoa, lakini ni kweli watoto wengi wa mwisho hudeka pia. Na hiyo ni changamoto tu kwetu
 
Hili lina ukweli ndani yake,yaani anaonekana kama mjukuu vile,limenikuta hili ila ntamnyoosha tu...khaa!
 
masaki tatizo hilo linauhusiano mkubwa na malezi ya familia aliyotokea binti huyo na kuwa wa mwisho si sababu ya msingi, kuna familia ambazo mzazi hana kauli juu ya mtoto humpa uhuru kuliko inavyotakiwa toka akiwa mdogo, kwa hiyo akifikia umri wa kuwa mke/mume hutaka yale malezi yaendelee, hapo ulitakiwa tangu wakati wa uhusiano kabla hajawa mke basi umuonyeshe msimamo wako kuwa hupendi tabia hiii na ile, na kumuonyesha tofauti ya kule kwa wazazi na hapo kwenu ambako yeye sasa ndio anakuwa mama kwa hiyo asitegemee kuendeleza tabia za kudeka au kujiamulia anachotaka, kila nyumba moja inatofautiana na nyingine, na ili nyumba iwe na nidhamu lazima kuwe na code of behaviour. kaa nae, mjiwekee rules za kuendesha nyumba yenu na umwambie in black and white kwamba now ameingia kwenye himaya nyingine na sio kwa wazazi wake alikotokea ajirekebishe ili asiwe kero, nachukia sana tabia ya kununa nuna kwenye ndoa... aaghhh!

mimi nimejaaliwa mtoto 1 tu tena wa kike na sitaki kabisa anizidi kauli maana najua nikiendekeza hilo atakuja kugeuka masikio ya punda atazidi kichwa na atakuja kushindikana kwenye ndoa.
 

Asante muhanga. Umenena vema sana! Wewe ni mmoja kati ya wana JF ambao ni nadra sana kupata ushauri wao, na pale unapopatikana, basi husheheni busara! Hapo kwenye bluu kwa kweli ni kero kubwa sana!
 
Asante muhanga. Umenena vema sana! Wewe ni mmoja kati ya wana JF ambao ni nadra sana kupata ushauri wao, na pale unapopatikana, basi husheheni busara! Hapo kwenye bluu kwa kweli ni kero kubwa sana!

thank you masaki. ukweli ni kero, tena hasa wanawake ndio tuna tabia hizo, natamani wangejua madhara yake wangeacha mara moja. wakati mwingine sie wenyewe huwa chanzo cha kuwafukuza waume nyumbani na wakishapotelea huko wanakopokelewa kwa bashasha tunaanza kulia na mto kitandani, wengine ndio kutafuta waganga na maombi ya mkesha... na hapo ndio huzidi kwenda 'chaka'
 
wa mwisho kama ni wa kiume hafai kuoa ila kuolewa kwa sababu atakuwa anadeka sana
 

Duh! Yaani matatizo unayatengeneza mwenyewe halafu unamsingizia ''shetani''! Ndio maana imeandikwa ''mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe''.
 
Duh! Yaani matatizo unayatengeneza mwenyewe halafu unamsingizia ''shetani''! Ndio maana imeandikwa ''mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe''.

na hapo Mungu hata ukimuomba ukiwa utupu hatajibu maombi yako!
 
Masaki hii inaweza kuwa kweli ila sio kwa wote so usigeneralize sema tu baadhi,na mi nafikiri kudeka ni hulka ya mtu.Mfano mie kwenye famikia yetu ni last born na huwezi jua hilo unless uambiwe and on the other side nina dada yangu anayenizidi 5 years anadeka kiasi unaezadhani ni last born.so it deep-ends
 

Very well said daughter. Hapo nimekuelewa 100%
 
sio wote wako hivyo,mim ni wa mwisho kwetu lkn siko hivyo,wote tumefundishwa kujituma na kujitegemea.
mwanamke mvivu ni mvivu tu hata akiwa wa kwanza au wa mwisho.
 
Kimsingi naona ni kama vile unakubaliana na mtoa mada, zaidi wewe umeongeza ukubwa wa seti kwa kuonesha aina nyingine ya wasichana ambao wanaweza kuwa wamedekezwa. Ukimsoma vizuri mtoa utaelewa kuwa anajaribu kusema kuwa wasichana waliodekezwa hawafai kuolewa, kwa kweli sina hakika sana na hili, na japokuwa ni kweli kuwa kudekezwa inaweza kutokea kwa mtoto wa namba yeyote kama ulivyojaribu kuainisha hapo juu lakini ni ukweli usiopingika kuwa watoto wanaodekezwa sana ni wale wa mwisho mara nyingi. Kwa hiyo basi kama ni kweli kuoa msichana aliyedekezwa ni mzigo, you will be running a huge risk of getting one of that type kama utaoa msichana ambaye ni wa mwisho.

OFF TOPIC:
Kwa upande mwingine tunaweza kujadili kama inafaa kuoa msichana aliyedekezwa.
 
Hao wanaosoma boarding tangu chekechea hata 0.5% ya watoto wote wa nchi hii hawafiki!

Kama ni asilimia ndogo hivyo inabidi iundwe tume ya kutathimini na ukweli utapatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…