Felixonfellix
JF-Expert Member
- Feb 16, 2010
- 1,672
- 183
sawa,ataitia doa shughuli, lakini hatazuia ndoa isifungwe. Mpe moyo kaka yako aache kulialia ,aendelee na maanadalizi ya arusi.mchungaji aarifiwe mapema kuhusu swala hilo.mtafute wifi yako mpe moyo ukiweza mpelekee na zawadi.siyo katoliki ni makanisa ya kiroho, ila anadai siku ya ndoa ataibuka kanisania siku hiyohiyo na mtoto mbele ya watu wote apinge si atatuharibi shughulu
hajawahi kuishi naye ni girl friend wa chuo waliachana tangu 2004, mwanamke ana mdomo balaa, anaongea wote tunajiona wadogo, anasema mtoto wake kakosa mapenzi ya baba ndo anatakiwa ayapate,, anamwambia mwenzake mimi nimezaa wewe hujazaa kaa pembeni watu walee mtot wao
haijarishi ni kanisa la aina gani au bomani au kwa shehe,
mtoto wa nje hazuii ndoa kufungwa
huyo mama anapaswa kuwa mpole kwa yote maana nafasi ya kuolewa allipoteza enzi hizo
kwa misingi hiyo hakuna sheria yoyote au ushahidi wowote wa kuweka pingamizi ati ndoa isifungwe. ukiweza printi hii michango ya wana JF umsomee au umpe asome mwenyewe na atajua ukweli halisi. hata kama unamuogopa bro, jivike ujasiri wa kumtia moyo.
Cha muhimu jitahidi kumtafuta huyo wifi mtarajiwa umtie moyo na umfariji.
hivi ni vijimambo tu vya wadandiao ndoa za watu.
sasa hii ya kuwa na illegitimate child imekuwa common ehh? ppl are not responsible at all and those poor kids have to pay... My heart goes to the kid poor little thing...
that was off topic... anyway back to the topic... naona huyo mchumba mwenyewe hana msimamo... kwanini anaanza kuzira?
hajawahi kuishi naye ni girl friend wa chuo waliachana tangu 2004, mwanamke ana mdomo balaa, anaongea wote tunajiona wadogo, anasema mtoto wake kakosa mapenzi ya baba ndo anatakiwa ayapate,, anamwambia mwenzake mimi nimezaa wewe hujazaa kaa pembeni watu walee mtot wao
DNA wamepima hospital tatu tofauti na majibu yanafanana, mtot ni wake maana wamefanana sana, ila binti anataka kuolewa, na huyu mwingine ameshikilia msimamo hataki, wivu na hasira vinamsumbua
Mkuu umeona kitu kikubwa sana katika maelezo ya jamaa.Hapa TZ hakuna hospitali inayopima DNA.
Mwenye kupinga ndoa ni mwanamke katika mazingira haya:
1. Mwanamke uliyeishi naye mfululizo kwa kipindi cha miezi sita (awali ilikuwa miaka miwili) na kuendelea na ambao mnafanya tendo la ndoa kama mume na mke, kusheria anatambulika kama mke hata kama hamjafunga ndoa, hivyo ni lazima muachane kisheria.
Mkuu..darasa limepita ila naomba tusahihishe kidogo.... unless unazungumzia sheria ya nchi nyingine... ya Tanzania haiko kama ilivyoelezewa hapo juu na hadi sasa kuna debates kali kujaribu kusukuma marekebisho ya LMA 1971- ila bado haijatokea.
Sheria ya Ndoa ya Tanzania ( Law of Marriage Act no.5 of 1971 - kuna ndoa za kufikirika - sijui kama ni kiswahili sanifu.. for Presumption of Marriage. Hii ni kama mwanamke na mwanaume wameishi kwa miaka miwili au zaidi.. katika mazingira ya kuifanya jamii iamini kuwa wao ni mke na mume basi there will be a rebuttable presumption that the couple are husband and wife.
Endapo basi kutatokea hali ya kuachana basi wana haki kudai kwa mfano walichochuma pamoja etc.Lengo la hii presumption hasa ni kuzuia watu wasi take advantage ya wengine kwa kuwafanya waamini kuwa wana mahusiano ya kindoa ilhali kuna utapeli.Ikitokea mmoja anataka kufunga ndoa mfano kanisani - maadam kanisa linakataza kuishi kinyumba bila ndoa basi mwenye kutaka kufunga ndoa hatakaliwa kufunga ndoa na mtu mwingine maana kuishi kinyumba siyo ndoa kufuatana na sheria za kanisa. Hali hii ilishawapata watu wengi hasa waliokuwa wanaishi kwenye mitala kienyeji au kimila..wakati wakristo hutambua ndoa ya mtu mke tu.
Nimeona nichangie kwa kuweka sawa msimamo wa kisheria.
Asanteni.