Mtoto wa nje kaja kujitambulisha!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Hebu tuchukulie kwamba, ukiwa umekaa nyumbani kwako, anafika mgeni. Huyu mgeni ni mtoto wa miaka 10 hivi. Mkeo anamkaribisha na anaingia sebuleni ulipo.

Anasalimia na baada ya salaam, mkeo anamuuliza shida yake. Kumbuka, mkeo ndiye aliyemkaribisha na kumuuliza maswali. Mtoto ni mtoto, kwani anasema wazi kwamba , ‘amekuja kwa baba yake' ambaye ni wewe.

Ina maana wewe ndiwe baba yake! Hukuwa hata siku moja maishani mwako umefikiria kwamba, ulikuwa na mtoto wa nje. Ghafla anakuja huyu mtoto na kusema mbele ya mkeo kwamba ni mwanao.

Hebu niambie, je ungekuwa ni wewe ungefanyaje?
 
Kama ulikuwa unafahamu kwamba una mtoto nje na hukuwa muwazi kwa mkeo, hilo litakuwa kosa kubwa sana kwa upande wako. Lakini kama ulikuwa huna habari na akaja mtoto, inabidi mmdadisi vema maana anaweza kuwa amekosea njia au nyumba.
 
Mtoto ni mtoto kama wa kwako mweleweshe mkeo ampokee,amlee kama wake!finished
 
Never leave any marks behind you if you are sure of not going back
 
kama ni wa kabla ya ndoa no problem. Wa baada ya ndoa kasheshe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…