Mtoto wa shule awekwa rumande wiki nzima bila kufikishwa mahakamani

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2007
Posts
2,903
Reaction score
1,360
Alifikishwa hapo polisi central mwanza jumamosi tar 10/8/2013 na hadi leo hii ijumaa tarehe 16/8/2013 bado yupo polisi.
Binti huyo wa miaka ipatayo 14 anayesoma suke ya sekondari Buhongwa kidato cha pili Jijini mwanza, amewekwa polisi central Mwanza kwa wiki nzima bila kufikishwa mahakamani wala kupewa dhamana ya polisi. Nimeweza kupata jina lake moja kuwa ni Mecktilda
Mama wa mtoto huyo ameonekana mara kwa mara kituoni hapo kujaribu kumtoa mwanae kwa dhamana ya polisi lakini hajafanikiwa.
Polisi hawataki kumfikisha mahakamani ili mahakama iamue kama kosa lake linastahili dhamana au la.
Mama huyo ambaye ni mjane anayefanya biashara ndogondogo ya kuuza ndizi, hivi sasa familia yake inaanza kuyumba kwani muda mwingi anautumia kufuatilia suala hili.
Wanajamii tusaidie suala hili; Najua hapa JF kuna wanasheria; ebu muone namna ya kumsaidia huyo mama na mwanae.
 
Mwambie aende mahakama ya wototo. Akaongee na watu wa ustawi wa jamii ambao wanaweza kumsaidia akaongea na hakimu. Hakimu anaweza kutoa order huyu mtoto afikishwe mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…